SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!
Maxence Melo akifikishwa mahakamani Ijumaa, Desemba 16, 2016. (Picha na Robert Okanda).
HomeJamii

SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!

Maxence Melo akifikishwa mahakamani Ijumaa, Desemba 16, 2016. (Picha na Robert Okanda) . Na Daniel Mbega HATIMAYE leo saa...

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA VIJIJINI DKT KIGWANGALLA AKABIDHI PIKI PIKI 19 MBELE YA KATIBU MKUU WA CCM, KINANA KWA WATENDAJI NA VIONGOZI WA KATA WA JIMBO HILO
AGGREY&CLIFFORD YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU, DAR
SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUWAONDOA VIJANA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI ILI WASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII










Na Daniel Mbega
HATIMAYE leo saa 5:15 asubuhi ya Jumatatu, Desemba 19, 2016 Maxence Melo ametoka kwa dhamana. Mungu ametenda.
Lakini ni baada ya Mkurugenzi huyo Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media Limited inayomiliki mtandao maarufu wa JamiiForums, kusota mahabusu kwa takriban saa 144 – yaani saa 72 katika mahabusu ya polisi na saa 72 nyingine kwenye Gereza la Mahabusu la Keko.

Hatimaye amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana katika kesi namba 457 ya mwaka 2016 ambayo iko mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, ambayo iliitwa tu kwa ajili ya kushughulikia dhamana.
Kesi hiyo imepangwa kuitwa Alhamisi, Desemba 29, 2016.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Msomi Mohammed Salum, uliieleza mahakama kwamba kesi hiyo ilikuwa imeitwa kwa ajili ya dhamana baada ya upande wa utete kushindwa kutimiza masharti ya dhamana wakati kesi hiyo iliposomwa kwa mara ya kwanza Ijumaa, Desemba 16, 2016.
Jopo la mawakili wa utetezi linaongozwa na Peter Kibatala, akiwa pamoja na Jeremiah Mtobesya, Benedict Ishabakaki, Jebra Kambole, Hassan Kyangiro na James Malenga, ambapo ilielezwa kwamba wadhamini wamepatikana na kukidhi vigezo vya dhamana ya maneno ya Shs. 5 milioni kila mmoja.
Hakimu Mwambapa alikubali kutoa dhamana na kumtaka mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.
Melo alikamatwa Jumanne, Desemba 13, 2016 saa 5 asubuhi – tena alikwenda mwenyewe baada ya kupigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Camillius Wambura.
Walichoelezwa hata waliokuwa wamekwenda naye ni kwamba, waondoke hapo polisi watakutana mahakamani kesho yake, yaani Desemba 14, 2016. Hakupelekwa mahakamani wala hakuchukuliwa maelezo.
Kwa siku mbili mfululizo kati ya Desemba 14 na 15 nilishinda katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati, jijini Dar es Salaam, nikiwa na wadau mbalimbali tukitafuta namna ya kumwekea dhamana. Haikuwezekana.
Hii ndiyo gharama ya kusimamia unachokiamini pamoja na maadili yanayokuongoza. 
Na wakati jitihada za kumpata mdhamini katika kesi mojawapo, upande wa Jamhuri ukawa umeondoka na wakati huo huo Maxence akapelekwa mahabusu ya Keko yapata saa 5 asubuhi. Hawakusubiri hadi saa 8 kama ilivyo kawaida ili kuwapandisha mahabusu wote kwenye karandinga, jambo ambalo likazua maswali mengi yasiyo na majibu.
Lakini hatimaye Max ameiona nuru, ambayo ameikosa kwa saa 144, japo kwa muda kwa sababu kesi hizi zinaendelea.
Kesi ya kwanza, ambayo ni namba 456, iko mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Thomas Simba, ambapo upande wa Jamhuri ulieleza kwamba, katika siku na tarehe tofauti kati ya Aprili 1, 2016 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni ndani ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd ambayo inaendesha mtandao wa JamiiForums, wakati akijua kwamba Jeshi la Polisi Tanzania linafanya upelelezi wa jinai kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa kwenye mtandao wake, kwa nia ya kuvuruga uchunguzi, alikaidi kwa makusudi amri ya kutoa taarifa ambazo alikuwa nazo, kinyume na kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crimes Law) namba 14 ya mwaka 2015.
Katika namba 457,  ambayo alikosa mdhamini, ilielezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwambapa kwamba, katika siku na tarehe tofauti kati ya Mei 10, 2016 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni ndani ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd ambayo inaendesha mtandao wa JamiiForums, wakati akijua kwamba Jeshi la Polisi Tanzania linafanya upelelezi wa jinai kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa kwenye mtandao wake, kwa nia ya kuvuruga uchunguzi, alikaidi kwa makusudi amri ya kutoa taarifa ambazo alikuwa nazo, kinyume na kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cyber Crimes Law) namba 14 ya mwaka 2015.
Aidha, katika kesi namba 458, ambayo iko mbele ya Hakimu Nongwa, Melo anakabiliwa na shtaka la kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini Tanzania (domain) kinyume na kifungu cha 79(c) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Namba 3 ya mwaka 2010 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 10 na 17 (4) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Namba 428 za mwaka 2011.
Upande wa Jamhuri ulieleza katika kesi hiyo kwamba, katika siku na tarehe tofauti kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13, 2016 katika eneo la Mikocheni ndani ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media Co. Ltd iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Kampuni (Sura ya 212 kama ilivyorejewa mwaka 2002) yenye hati ya usajili Namba 66333 amekuwa akiendesha na kutumia tovuti inayojulikana kama jamiiforums.com ambayo haijasajiliwa kwenye code za Tanzania (country code Top Level Domain - ccTLD), inayofahamika kama do-tz.
Yaliyompata Max ni mwanzo tu wa yale ambayo yanaweza kutupata sote, hususan waandishi wa habari wa mtandaoni na watumiaji wengine wa mitandao.
Hii inatokana na kuwepo kwa Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Cyber Crimes Law) ya mwaka 2015, ambayo ilipitishwa Aprili Mosi, 2015.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!
SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgedTgPEz34zscbrwNxeG7b1COEdtTARAPeh9eXd2gk7rgdZ3DXJkk1OqM2dbbsALUGF4dkadJkrnLj6Iv5pW7Oz5s__n51se3BwnEBltDxk18xjw3RURoC_AArwMYve6SXMP6CZQMBJNg/s640/melo.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgedTgPEz34zscbrwNxeG7b1COEdtTARAPeh9eXd2gk7rgdZ3DXJkk1OqM2dbbsALUGF4dkadJkrnLj6Iv5pW7Oz5s__n51se3BwnEBltDxk18xjw3RURoC_AArwMYve6SXMP6CZQMBJNg/s72-c/melo.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/saa-144-za-maxence-melo-ndani-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/saa-144-za-maxence-melo-ndani-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy