BALOZI WA KUWAIT, JASEM AL-NAJEM AZINDUA VISIMA VINNE KATIKA SHULE NNE ZA MSINGI MANISPAA YA ILALA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Da...


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam jana.

Shule za Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja, Mwale pamoja na Bwawani

Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndio maana wameona umuhimu wa visima hivyo katika shule hizo.

Amesema wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.

Al-Najem amesema kuwa wamefanikiwa kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 63,000 na watu wengine wanaweza kujitokeza kusaidia jitihada mbalimbali .

Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani sh.milioni tatu.
 
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji katika shule ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jana, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem kushoto na Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi wakinywa maji mara baada kuzindua kisima katika shule ya msingi Yombo jana jijini Dar es Salaam. 

Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo jana jijini Dar es Salaam.
 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam. 
 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.
 
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akimsikiliza Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
 

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA KUWAIT, JASEM AL-NAJEM AZINDUA VISIMA VINNE KATIKA SHULE NNE ZA MSINGI MANISPAA YA ILALA
BALOZI WA KUWAIT, JASEM AL-NAJEM AZINDUA VISIMA VINNE KATIKA SHULE NNE ZA MSINGI MANISPAA YA ILALA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggTjFxGZ7FQcP2a_FjXDZrUc4cuVDdbfW2aSJoYrUubJLgweYRJkADIska8tBdLgZGBo3tvw2wKil34CyTDVqxG0FBo3dWMo2amEbB8IWlS6Kb9N4Mao-H2WnggR9z2MTwoMPnYvkJAbE/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggTjFxGZ7FQcP2a_FjXDZrUc4cuVDdbfW2aSJoYrUubJLgweYRJkADIska8tBdLgZGBo3tvw2wKil34CyTDVqxG0FBo3dWMo2amEbB8IWlS6Kb9N4Mao-H2WnggR9z2MTwoMPnYvkJAbE/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/balozi-wa-kuwait-jasem-al-najem-azindua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/balozi-wa-kuwait-jasem-al-najem-azindua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy