Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akikabidhiwa funguo za jengo la hosteli la...
|
Jengo jipya
la hosteli ya wasichana la Chuo cha Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake
umemalizika hivi karibuni.
|
Jengo jipya
la hosteli ya wasichana la Chuo cha Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake
umekamilika hivi karibuni.
|
Moja ya
chumba katika jengo lililokabidhiwa la hosteli ya wasichana ya Chuo cha Madini
(MRI) Dodoma.
|
Bwalo la
wanafunzi wa chuo cha Madini Dodoma baada ya kukarabatiwa na kupanuliwa.
|
Wizara
ya Nishati na Madini imepokea jengo la hosteli ya wasichana ya Chuo, cha Madini
cha Dodoma (MRI) kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Chichi Engineering
Construction Limited katika makabidhiano yaliyofanywa hivi karibuni, mkoani
Dodoma mara baada ya ujenzi kukamilika.
Akizungumza
kwa niaba ya Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali
Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahya, wakati wa makabidhiano hayo Msanifu
Majengo (Architect) wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi
huo kutapunguza uhaba wa nafasi za malazi kwa wanafunzi hususan wa kike katika
chuo hicho
Aidha
alisema kulingana na takwimu za MRI inaonyesha kila mwaka usaili wa wanafunzi
unaongezeka na kwakua chuo hicho hakina hosteli za kutosha inawalazimu
wanafunzi wengi kupangisha vyumba nje ya chuo jambo ambalo alisema si jema kwa
wanafunzi hao.
"Kila
mwaka wanafunzi wanaongezeka, kwahiyo kupitia jengo hili jipya la hosteli ya
wasichana nina imani changamoto ya malazi kwao itakua imetatuliwa,"
alisema.
Katika
makabidhiano hayo, ilielezwa kuwa jengo hilo la hosteli linao uwezo wa kuchukua
jumla ya wanafunzi 88.
Aidha,
mbali na jengo hilo la hosteli, makabidhiano hayo pia yalihusu ukarabati na
upanuzi wa bwalo la wanafunzi pamoja na ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Chuo.
Arch. Ringo
alieleza kuwa makabidhiano hayo yanakamilisha Awamu ya kwanza ya Mradi wa SMMRP
kwa chuo hicho na alisema matarajio ya baadaye ni kujenga miundombinu zaidi ili
kukidhi mahitaji ya chuo hicho.
"Mahitaji
ya chuo kuhusiana na majengo ni makubwa kuliko haya yaliyojengwa,"
alisema.
Akizungumzia
mikakati ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mradi wa SMMRP (Additional
Financing), Arch.Ringo alisema hatua zote za kuanza utekelezaji zimeanza.
"Matarajio
yetu ni kuwa malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa muda uliopangwa. Mradi huu
umebeba dhima kubwa ya kuhakikisha Watanzania wananufaika zaidi na sekta
ya Madini," alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha Madini, Mhandisi Oforo Ngowi, alisema
mradi huo wa ukarabati na ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Chuo, bwalo la wanafunzi
na hosteli unao umuhimu wa kipekee katika kuboresha miundombinu pamoja na
kuleta maendeleo endelevu ya chuo hicho.
"Huu
ni ukombozi mkubwa sana kwa wanafunzi waliokuwa wanahangaika kutafuta malazi
nje ya chuo. Kilichobaki ni hapa kusoma tu," alisema.
Mradi
huo wa Chuo cha Madini uliokabidhiwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya
usimamizi wa SMMRP na ulianza Julai, 2014 na kukamilika mwaka huu 2016 na
ilielezwa kwamba umegharimu takriban milioni 997.
Aidha
jengo hilo la hosteli limebuniwa na kampuni ya ubunifu Majengo ya PSM
Architects Ltd kwa kushirikiana na Howard Humphreys (T) Ltd na Mas-Q Associates
Ltd.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi zinazotekeleza miradi mbalimbali ya sekta ya madini chini
ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
COMMENTS