Mshambuliaji wa Yanga, Jenilson Santos 'Jaja' akijikunja kupiga shuti mbele ya beki wa Tanzania Prisons, wakati wa mche...
Mshambuliaji
wa Yanga, Jenilson Santos 'Jaja' akijikunja kupiga shuti mbele ya beki
wa Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambapo bao la
kwanza la Yanga lilifungwa na Andrey Coutinho katika dakika ya 38, bao
la pili lilifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 69, huku bao la
Prisons likifungwa na Ibrahim Kahaka, katika dakika ya 67.
Beki wa Tanzania Prisons, akiokota mpira wavuni hili lilikuwa ni bao la kwanza.
Simon Msuva (kulia) akijaribu kutoka beki wa Tanzania Prisons, Nurdin Chona, wakati wa mchezo huo.
Simon Msuva (kushoto) akikimbia kushangilia bao lake alilofunga katika dakika ya 69.
Sehemu ya mashabiki wa Tanzania Prisons....
Jenilson Santos 'Jaja' (kulia) akijaribu kupiga shuti mbele ya mabeki wa Prisons. Lugano Mwangama na Nurdin Chono.
COMMENTS