TIMU YA WATOTO WA MTAANI YA TANZANIA YAREJEA NCHINI NA KOMBE LA DUNI KATIKA MCHEZO WA SOKA Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaan...
TIMU YA WATOTO WA MTAANI YA TANZANIA YAREJEA NCHINI NA KOMBE LA DUNI KATIKA MCHEZO WA SOKA
Wachezaji
wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia
katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za
watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano
hayo.
Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza
Alfat Mansoor (Dogo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo
kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es
Salaam.
Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka
Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kwa kufunga magoli 3-1 dhidi ya
Burundi Frank William (mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji
wenzake mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Nyerere juzi. Kushoto ni Hassan Jaffar, Emmanuel Amos,
na Hassan Seleman.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana
Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa dunia mara baada ya kuwapokea wachezaji wa timu ya
watoto wa mitaani ya Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu
kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya
saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka. (Picha zote na Frank Shija, Afisa Mawasiliano Serikalini)
COMMENTS