WAZIRI MKUU MAJALIWA AUNGANA NA WAUMINI WA KIISLAMU DODOMA KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Okt...

















Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika Dua ya kuwaombea wanafunzi wote wa Tanzania wanaotarajia kufanya mtihani wa Kidato cha Nne ili wafanye vizuri akiwa katika  Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakiomba dua mara baada ya sala ya Ijumaa ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alihutubia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam baada ya Sala ya Ijumaa.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba  na Sheikh Shabaan Kitila baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Nunge mjini Dodoma Oktoba 28, 2016


 TUMIENI MISIKITI KUHUBIRI MISINGI YA UISLAMU-MAJALIWA



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Waislamu watumie nyumba za ibada kuhubiri uislamu na misingi yake.



Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Oktoba 28, 2016) wakati akishiriki sala ya Ijumaa katika msikiti wa Nunge mjini Dodoma.



Amesema dini ya Kiislam inafundisha kwamba sala ndiyo msingi mkubwa unaopaswa kufuatwa na kila muumini hivyo ni lazima wafanye ibada kwa wakati.



“Nasisitiza kwamba wote tutumie muda wetu vizuri pamoja na mambo mengine tufanye ibada kwani dini inatuekeza kuwa sala ndiyo msingi mkubwa kwenye Uislamu. Tunayo kazi ya kuimarisha misingi ya dini kwa kutumia nyumba za ibada,” amesema.



Waziri Mkuu amesema Waislamu wana jukumu la kufundisha watoto wao na kuhakikisha wanakua kwenye imani na kujengeka katika maadili mema.



“Dini inajenga maadili mema kwa mtoto na hata mtu mzima. Pia dini inajenga misingi ya uvumilivu na inamuwezesha mtu kumtambua Mwenyezi Mungu. “Tuendelee kuwafundisha vijana wetu umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kidini ili wakikua waweze kuiendeleza kwa vizazi vijavyo,” amesema.



Waziri Mkuu ambaye ametumia fursa hiyo kujitambulisha kwa waumini wenzake wa mkoa wa Dodoma baada kuhamia rasmi, ameahidi kutoa ushirikiano kwao na pia amewaomba wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.



“Nimekuja kujitambulisha. Mimi ni kijana wenu, ndugu yenu. Nimekuja Dodoma rasmi  nyumbani na  kikazi. Naomba mnipokee na naamini katika kipindi chote nitakachokuwa hapa nitapata ushirikiano nanyi na pia nitawapa ushirikiano,” amesema.



Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwaomba waumini hao wawaombee dua wanafunzi wa kidato cha nne ambao wanatarajia kuanza mitihani ya kuhitimu Novemba Mosi,  mwaka huu ili waweze kufaulu.



Waziri Mkuu amewaomba waumini hao waendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao na kufikia malengo yanayotarajiwa na wananchi.



Aidha, Waziri Mkuu amechangia sh. milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa zahanati katika msikiti huo. Miradi inayojengwa na waumini wa msikiti huo kwa sasa ni zahanati, madarasa ya shule ya awali na shule ya ufundi.



  

                            

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.
IJUMAA, OKTOBA 28, 2016.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU MAJALIWA AUNGANA NA WAUMINI WA KIISLAMU DODOMA KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA
WAZIRI MKUU MAJALIWA AUNGANA NA WAUMINI WA KIISLAMU DODOMA KATIKA IBADA YA SALA YA IJUMAA
https://i.ytimg.com/vi/Ahn-DSBa8j8/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/Ahn-DSBa8j8/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/waziri-mkuu-majaliwa-aungana-na-waumini.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/waziri-mkuu-majaliwa-aungana-na-waumini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy