JOKATE KUIJENGEA UWANJA WA MICHEZO SHULE YA SEKONDARI MAJANI YA CHAI

Jokate Mwegelo akiwasili katika shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya Vingunguti jijini Dar es Salaam juzi. Kulia kwake ni...







Jokate Mwegelo akiwasili katika shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya Vingunguti jijini Dar es Salaam juzi. Kulia kwake ni Mkuu wa shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.
 
 
 
 


Jokate Mwegelo akitoa hotuba yake katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne ya Shule ya secondari ya Majani ya Chai. Katika Hotuba yake, Jokate alitoa ahadi ya kuwajengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo shuleni hapo. Ujenzi huo utaanza baadaye.
 
 
 

Mkuu wa Shule ya ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kasango Pascal Ngozi akitoa neno la shukrani baada ya ahadi ya Jokate Mwegelo wa kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.
 
 
 

Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. 
 


Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (kulia) ni mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi. 
 
 


Jokate Mwegelo akiserebuka na wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane yaliyofanyika juzi. Jokate ameahidi kuijengea shule hiyo uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.




Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga uwanja wa michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini.

Akizungumza katika Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

Jokate ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.

“Nashukuru kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.

Alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.

Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia viwanja vya shule jirani katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni moja ya masomo muhimu sana.Ngozi alisema kuwa wanatambua kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule yao, lakini kutokana na kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.

“Tunashukuru Jokate kwa ahadi ya kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo, hii itatoa hamasa kwa wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali kutambuliwa na vile vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la utawala, samani za ofisini na kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau watusaidie kufanikisha hayo,” alisema Kasango.

Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.Kati ya wanafunzi zaidi ya 290 wanaomaliza kidato cha nne, Khalid Ibrahim alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora huku Latifa Kihiyo akitwaa tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: JOKATE KUIJENGEA UWANJA WA MICHEZO SHULE YA SEKONDARI MAJANI YA CHAI
JOKATE KUIJENGEA UWANJA WA MICHEZO SHULE YA SEKONDARI MAJANI YA CHAI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlA82YlTsT6p8B7fFMcEtzWeDeF0FX3FA9mrPu-83aiybKLQGEy4ynaWf-_NVed4izjs8MGGz3hnU6xq91bMsyLxsXjm2WAn2xrlIXXH2LL7ZlsEqnRXvXTYxk6e0sxhSUc0Ew8vdQNvQT/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlA82YlTsT6p8B7fFMcEtzWeDeF0FX3FA9mrPu-83aiybKLQGEy4ynaWf-_NVed4izjs8MGGz3hnU6xq91bMsyLxsXjm2WAn2xrlIXXH2LL7ZlsEqnRXvXTYxk6e0sxhSUc0Ew8vdQNvQT/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/10/jokate-kuijengea-uwanja-wa-michezo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/jokate-kuijengea-uwanja-wa-michezo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy