TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA MAAFA

Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akieleza umuhimu wa makazi salam...






Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akieleza umuhimu wa makazi salama wakati cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa yenye Kaulimbiu “MAKAZI SALAMA:Punguza Makazi katika maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama Kutokana na Maafa” yaliyoadhimishwa katika Viwanja vya Nyerere Square Dodoma Oktoba 13, 2017.


Mratibu Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Edger Senga akizungumza jambo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Oktoba 13, 2017 mjini Dodoma.


Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Chamwino B wakisoma shairi kwa mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu tarehe 13, Oktoba, 2017 Mjini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akitoa zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya msingi Chamwino B walioshiriki katika kusoma shairi lenye kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ambayo inasema “MAKAZI SALAMA:Punguza Makazi katika maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama Kutokana na Maafa” mjini Dodoma Oktoba 13, 2017.


Mwalimu wa Shule ya Msingi Makole Habiba Seifu akipokea zawadi ya ushiriki wa shule yake kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa yanayoadhimishwa kila tarehe 13 Oktoba,2017.

Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu (katika) akifuatilia shairi kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi Makole (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maaf yanayoadhimishwa kila tarehe 13 Oktoba,2017 Duniani. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Frank Mvungi- Maelezo Dodoma
Serikali yapima Viwanja zaidi ya milioni moja na nusu katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini ikiwa ni moja ya mikakati ya kuondoa makazi holela na kuepusha maafa yanayotokana na matumizi ya ardhi yasiyozingatia sheria kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya Ardhi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Masaidizi Idara ya Uratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa yaliyofanyika Kitaifa mjini Dodoma na Kuwashirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali.
“Wananchi wazingatie sheria,Kanuni, na Taratibu kwa kuepuka kujenga maeneo hatarishi kama mabondeni,maeneo yenye mafuriko na mengine yote yanayokatazwa kisheria ili kuepuka maafa” Alisisitiza Taratibu
Akifafanua Taratibu amesema kuwa Viongozi wa Serikali katika maeneo yote hapa nchini wanajukumu la kusimamia sheria zilizopo ili kuepusha maafa kwa kuzingatia Kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “MAKAZI SALAMA: Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi,Punguza kuhama kutokana na maafa”.
Akizungumzia mikakati ya Serikali kuondoa maafa na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa maafa amesema kuwa Idara ya Maafa imekuwa ikitoa elimu kwa Umma ili kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa utakaosaidia kuepuka athari za maafa.
Aidha alitaja hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali kuwa ni kutungwa kwa sheria ya maafa ya mwaka 2015, Miongozo,Kanuni na kuwekwa kwa taratibu mbalimbali za kusimamia masuala ya maafa hapa nchini.
Kwa upande wake mratibu wa maafa Wilaya ya Chamwino Bi Lilian Zakaria amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Vijjiji wakishirikisha Kamati za Maafa katika ngazi zote ili kuwajengea wananchi uwezo wa kupambana na maafa pale yanapotokea na pia kuzuia viashiria vyake.
Pia Bi Zakaria amewataka wananchi kuepuka kujenga na kuishi katika maeneo hatarishi na kuzingatia taratibu zote zilizowekwa na Serikali kuepuka maafa.
Naye Mwakilishi wa Asasi za Kirai Bw. Mussa Mussa amesema kuwa wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na maafa hali inayosababisha wananchi kuishi salama katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Chimbuko la Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ilitokana na Azimio Na. 64/200 lililopitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa tarehe 21 Desemba, 2009 ambapo iliamuliwa Oktoba 13 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa ikiwa na lengo la Kukuza utamaduni wa kupunguza madhara ya maafa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuzuia, kupunguza madhara, Kujitayarisha, Kukabili na Kurejesha hali kuwa bora zaidi na mwaka huu kaulimbili inasema:“MAKAZI SALAMA: Punguza Makazi katika Maeneo Hatarishi, Punguza Kuhama kutokana na Maafa”

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA MAAFA
TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA KUPUNGUZA MAAFA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/10/P1-1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/tanzania-yaadhimisha-siku-ya-kimataifa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/tanzania-yaadhimisha-siku-ya-kimataifa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy