SIMBA YATAFUNA MUWA WA MTIBWA SUGAR 2-0 Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akiwania mpira na beki wa M...
SIMBA YATAFUNA MUWA WA MTIBWA SUGAR 2-0
Kiungo
Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akiwania mpira na beki wa
Mtibwa Sugar, Shaban Nditi, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom,
uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini dar es Salaam. Katika
mchezo huo, Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-0.
************************************
BAO
la dakika ya 90+, lililofungwa na Betram Mwombeki, limeiwezesha timu ya
Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom, dhidi ya Mtibwa Sugar, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Henry
Joseph, aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Said Hamis, katika dakika
ya 67.
HUKO KWINGINEKO:- COASTAL UNION -0 PRISONS- 0
RUVU SHOOTING -1 MGAMBO SHOOTING- 0
JKT-1 ASHANTI UNITED- 0
YANGA-1 MBEYA CITY-1
AZAM-1 KAGERA SUGAR-1
OLJORO-1 RHINO RANGERS 1
Mshambuliaji
wa Simba, Amis Tambwe (kushoto) akijiandaa kupiga shuti, huku akibanwa
na beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Mbeikya, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba, wakishangilia bao la pili.
Mfungaji wa bao la kwanza la Simba, Henry Joseph (kulia) akiwafinya mabeki wa Mtibwa Sugar.
Beki wa Simba Issa Rashid (kulia) akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari. (PICHA NA SUFIANI MUHIDINI)
LOWASSA ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MTEMI ISIKE MWANAKIYUNGI WA KABILA LA UNYAMWEZI, MKOANI TABORA JUMAMOSI
Waziri
Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
akisalimiana na Machifu mbalimbali kutoka sehemu tofauti tofauti hapa
nchini, wakati akiwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya Kumbukumbu ya
Mtemi Isike Mwanakiyungi wa kabila la Unyamwezi aliefariki Miaka 124
iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika kwenye Kijiji cha Itetemya, Mkoani
Tabora. Kushoto ni Chifu Mkuu wa Unyanyembe, Chifu Msagata Fundikira.
Waziri
Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
akifurahia jambo na Mjukuu kutoka katika Ukoo wa Fundikira. Kushoto ni
Chifu Mkuu wa Unyanyembe, Chifu Msagata Fundikira.
Waziri
Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
akiangalia Ngoma za Asili ya Kabila la Unyamwezi waliokuwa wakitoa
Burudani kwenye Sherehe hizo.
Mmoja wa Machifu wa Unyanyembe akimkabidhi zawadi ya Asali,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
akionyeshwa moja ya kibuyu cha Tambiko la Kabila la Unyamwezi.
Chifu
Mkuu wa Unyanyembe,Chifu Msagata Fundikira akifanya tambiko muda mfupi
kabla ya kumtawaza kuwa mmoja wa Machifu wa Unyanyembe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia)
akisikiliza kwa makini wasifu wa Marehemu, Mtemi Isike Mwanakiyungi
aliyefariki Miaka 124 iliyopita. Wasifu huo ulisomwa na Richard
Mchembe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa pamoja na
Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe, Chifu Msagata Fundikira
wakishirikiana kuweka jiwe la msingi katika eneo litakalojengwa mnara wa
kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi aliyefariki miaka 124
iliyopita. Sherehe hizo zimefanyika kwenye Kijiji cha
Itetemya, Mkoani Tabora.
COMMENTS