Taasisi ya Elimu ya Watu wazima yaendelea Kujizatiti katika kutoa elimu bora kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi ili waweze kuch...
Taasisi ya Elimu ya Watu wazima yaendelea Kujizatiti katika kutoa elimu bora kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi ili waweze kuchangia katika kujenga uchumi wa Viwanda.
Kaimu Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Kassimu Nihuka amesema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa kufunga warsha ya uandaaji wa mihtasari ya Fizikia na kemia iliyowashirikisha walimu wa masomo hayo kutoka baadhi ya shule za sekondari za jijini Dar es Salaam
“Katika kuboresha utoaji wa Elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi ilishakamilisha uandishi wa mihtasari ya masomo ya Hisabati, Biolojia, Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili na Kiingereza na ambayo inatumika katika vituo vinavyotoa elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi mikoa yote nchini. “ Alisisitiza Dkt. Nihuka
Kupitia jukumu la kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi TEWW imesajili jumla ya vituo 547, kati ya hivyo 93 vinaendeshwa na TEWW na vingine 454 vinaendeshwa na wadau. Jumla ya wanafunzi 10,420 wakiwemo wanawake 6,074 (58.3%) na wengine 4,346 (41.7%) wanaume wanasoma elmu ya sekondari nje ya mfumo rasmi nchi nzima kwa kutumia mitaala iliyoandaliwa na TEWW.
Ili kuwajengea wanafunzi msingi wa masomo ya sayansi hususani Fizikia na Kemia, TEWW imeandaa mitaala ya masomo haya itakayotumika katika kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi. Kwa sasa wanafunzi wetu wa sekondari wanasoma masomo saba likiwemo somo la bailojia pamoja na Hesabu. Uandaaji wa mitaala ni moja ya majukumu ya TEWW kisheria.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Namba 12 ya mwaka 1975 na kupewa majukumu mbalimbali.Pamoja na majukumu mengine, Taasisi inajukumu la kutoa elimu ya sekondari kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa pamja na mafunzo ya jioni pamoja na kuandaa mitaala kwa ajili ya kutoa elimu nje ya mfumo rasmi.
Wataalamu wa Uandaaji wa Mitaala ya masomo ya Fikizia na Kemia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) Dkt. Kassimu Nihuka (hayupo pichani) Jijini Dar es Salaam. |
COMMENTS