SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRID YA TAIFA Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) l...
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRID YA TAIFA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
linawataarifu Wateja wake na Umma kwa ujumla kuwa kumetokea hitilafu
katika Kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza Umeme cha Ubungo, hitilafu
hiyo imesababisha Grid ya Taifa kutoka na kusababisha Mikoa yote
iliyounganishwa katika Grid ya Taifa kukosa Umeme.
Mafundi wanaendelea na jitihada ya kurejesha Umeme katika hali yake ya kawaida.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.
Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
COMMENTS