SBL YAWAPATIA WATANZANIA MILIONI MBILI MAJI YA UHAKIKA, SALAMA
 Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi  kwa  waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia Watanzania milioni 2 katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema jana  katika hoteli ya Morena Mkoani Dodoma.
HomeJamii

SBL YAWAPATIA WATANZANIA MILIONI MBILI MAJI YA UHAKIKA, SALAMA

 Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi  kwa  waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia W a...

UNESCO YAFANYA UZINDUZI WA KOZI YA MAADILI KWA WALIMU WA VYUO VYA AFYA NA SAYANSI
MAMBO MBALIMBALI YALIYOFANYIKA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
MAONYESHO YA BIDHAA YA VYAKULA KUTOKA INDIA YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM






Waandishi wa habari wa mkoani Dodoma wakichukua matukio wakati wa mkutano uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena mkoani Dodoma.

Moja ya mradi wa maji uliodhamiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited  uliozinduliwa mapema Novemba mwaka jana katika Kijiji cha Makanya wilayani Same katika  programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo  inayolenga kuboresha maisha.



Dodoma, Januari 24, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi ya  milioni mbili kote nchini maji safi na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita  kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo  inayolenga kuboresha maisha.

 Kupitia programu yake inayofahamika kama Maji kwa Uhai, SBL imechimba visima vya kisasa 16 katika mikoa minane na kuwezesha jamii  katika maeneo hayo  kupata maji ya uhakika na salama.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha  alisema kwamba kampuni hiyo ya bia  imejikita katika kupunguza uhaba wa maji katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitaabika kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

 “SBL  ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya Maisha  ikiwa ni moja ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu  imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua  maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Wanyancha aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji  kuliko kusafiri umbali mrefu  kutafuta maji.

Aliongeza, “licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya jamii  unahakikisha kuwa watoto hususani watoto wa kike  wanaosoma shule  wanapata muda  mzuri wa  kuhudhuria  shuleni kwa uhuru zaidi bila usumbufu”.

Mkurugenzi huyo wa Mahusiano  alieleza kwamba mpango wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni  kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha, Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha  wakazi zaidi ya 300,000.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SBL YAWAPATIA WATANZANIA MILIONI MBILI MAJI YA UHAKIKA, SALAMA
SBL YAWAPATIA WATANZANIA MILIONI MBILI MAJI YA UHAKIKA, SALAMA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrbnkC80A4_autCmp0hc1p3e7Vv5-xf77WOiW0lxsAvARRIIDMMwTcWVfdGEhEwb-wndqupnnkDs0Lc76_kCJQ64zijkKvW6KMkZP9_rpFX3p6n-_Ja6yOxJmfSvqFESBpCI2m8s_ViXQ/s640/IMG_7312.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrbnkC80A4_autCmp0hc1p3e7Vv5-xf77WOiW0lxsAvARRIIDMMwTcWVfdGEhEwb-wndqupnnkDs0Lc76_kCJQ64zijkKvW6KMkZP9_rpFX3p6n-_Ja6yOxJmfSvqFESBpCI2m8s_ViXQ/s72-c/IMG_7312.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/sbl-yawapatia-watanzania-milioni-mbili.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/sbl-yawapatia-watanzania-milioni-mbili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy