MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO
HomeJamii

MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Ma...

RAIS DKT. MAGUFULI AKIANGALIA KIATU KINACHOTENGENEZWA NA KIWANDA CHA MAGEREZA CHA KARANGA
RAIS DKT. MAGUFULI ATIA SAINI NYARAKA ZA MSAMAHA WA WAFUNGWA 63 AMBAPO 61 WALIKUWA WA KUNYONGWA NA MAJINA MAWILI (2) YA WAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA.
RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo.
 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya
Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari)
Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa kikao
kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na Afisa Utumishi wa manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma akishauri jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo.

 


Usikivu ni jambo la busara kikaoni.
 
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa ya Ubungo.

 


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewataka wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao za uongozi kwa kuwatumikia wananchi kwa haki huku akiwasihi kuishauri serikali katika majukumu yake ili kuwa na maendeleo chanya katika maeneo yao sawia na kupunguza lawama za mambo yaliyopita ili kuwa na Manispaa imara yenye ukusanyaji mzuri wa mapato.

MD Kayombo amewasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Mitaa.

MD Kayombo ameyasema hayo Wakati wa kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo wenyeviti wote wamekabidhiwa Bendera, Rejista, Vitini vyenye miongozo ya kisheria sambamba na vitini vinavyobainisha majukumu ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kutoingiliana katika utendaji na viongozi wengine wakiwemo watendaji wa Mitaa na Kata.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa wenyeviti wanapaswa kuwasimamia vyema wananchi kulipa kodi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya Manispaa kujisimamia yenyewe na kujiendesha kirahisi.

Mstahiki Meya ametumia Kikao hicho kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg John Lipesi Kayombo kwa uongozi wake imara na uliothubutu kwani umewafanya wananchi katika Manispaa hiyo kuwa walipaji wazuri wa kodi.

Jacob amesema kuwa mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya mfano na kuzishinda Manispaa zingine katika Jiji la Dar es salaam.

Kuhusu Posho za wenyeviti wa Mitaa, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewasihi wenyeviti kuwa na subira kwani wanaandaa mpango imara kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuwalipa malimbikizo ya posho zao zote wanazodai.

Pia amewasihi wenyeviti hao kutumia Uhuru wao kikatiba kuwafungulia kesi wale wote wanaowaonea, kuwazalilisha na kuwakejeli kwa kuwafungulia kesi katika mahakama kwa mujibu wa sheria.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO
MD KAYOMBO: YALIYOPITA SI NDWELE TUGANGE YAJAYO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhNvGMZ4NHHU9NrSEAEkrzC3RMJu2IUcPq6wudlCLYQeaPdDwSl8qyu1e2B-HiGLL2SHN1AqfV-wG1LZjjh8_mtcnSV-md7r-A2vAMFzQG7k_pnngWCFhBzUXu5biftTRV4Jqm_DNfi7Jg/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhNvGMZ4NHHU9NrSEAEkrzC3RMJu2IUcPq6wudlCLYQeaPdDwSl8qyu1e2B-HiGLL2SHN1AqfV-wG1LZjjh8_mtcnSV-md7r-A2vAMFzQG7k_pnngWCFhBzUXu5biftTRV4Jqm_DNfi7Jg/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/md-kayombo-yaliyopita-si-ndwele-tugange.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/md-kayombo-yaliyopita-si-ndwele-tugange.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy