KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI
HomeJamii

KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI

 Kikosi kazi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika Morogoro

JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 159
RED CROSS YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA IDARA YA MAAFA
RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA NMB







 Kikosi kazi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika Morogoro



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania Dkt. Stephen Nindi akichangia jambo wakati wa mkutano huo.

 Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano huo
 Bw. Marcely Madubi kutoka Asasi ya kiraia ya Care International  (wa pili kulia) akichangia jambo katika kipengele cha Changamoto na mapendekezo kuhusu upangaji , utekelezaji na usimamizi wa mipango na matumizi ya Ardhi
 Bw. Jamboi Baramayegu kutoka Ujamaa-CORT akichangia jambo juu ya hangamoto na mapendekezo katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya Ardhi.

 Bw. Gerald Mwakipesile Afisa  Mipango wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akizungumza juu ya Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu maswala
mbalimbali yanayokabili upangaji,utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya Ardhi nchini.
Mratibu wa Mradi wa Ardhi yetu kutoka Asasi ya Kiarai ya Care International Bi. Mary Ndaro akizungumzia jambo juu ya Taasisi zinazojihusisha na Mipango ya matumizi za Ardhi nchini na kusisitiza ushirikiano.

 Bw. Paulo Tarimo ambaye ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akitolea msisitizo Jambo.
Profesa Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo Akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa mkutano huo
Mmoja wa washiriki katika Mpango kazi akifafanua jambo.

Mwakilishi kutoka Asasi ya Kiraia ya kimataifa Oxfam Naomi Shadrack akichangia jambo wakati wa Mkutano huo.
Profesa Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu wa Kitivo cha Usanifu Majengo akipitia kuona kazi zinavyofanyika katika makundi mbali mbali.
Majadiliano katika Makundi Mbalimbali yakiendelea

(Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa)



Wadau mbalimbali wa Mashirika ya Kiraia na Sekta binafsi kwa kushirikiana na TUME  ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wanatarajia kukabidhi  ripoti  maalum kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,William Lukuvi ifikapo Desemba mwaka huu ripoti  hiyo ikiwa ni ya uandaaji wa mpango kazi wa utekelezaji wa Makubaliano ya Mkutano mkuu wa Wadau wa
Mipango ya Matumizi ya ardhi nchini .
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kikosi kazi uliofanyika mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi  ya Ardhi, Dk Stephen Nindi alisema vitu muhimu katika nchi ambavyo vinasaidia kupunguza kwa  kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ni upangaji wa matumizi bora ya ardhi.

Alitaja vitu ambayo ni miongoni vinavyokwamisha kwenda kwa kasi kwa zoezi la upangaji wa matumizi bora ya ardhi ni pamoja na ufinyu wa bajeti na ukosefu wa
teknolojia mpya zinazoweza kupima na kupanga ardhi kwa mwendo wa haraka zaidi.

Aidha Dkt. Nindi alisema Kikosi kazi hicho kilikutana katika mkutano huo kwa lengo la kuandaa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kumfikia Waziri Mh. Lukuvi na kuona ni namna gani nchi nzima  inafanikiwa kuwa na mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro iliyopo sehemu mbalimbali nchini.
Alisema viongozi wa kitaifa wanapaswa kutambua kwamba ardhi ni suala nyeti  na mtambuka hivyo wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mipango ya
matumizi bora ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaweza kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi inayojitokeza. "Tunatarajia kufikisha ripoti hii kwa Muheshimiwa Waziri Lukuvi na yeye ataona ni namna gani atakavyowashirikisha Mawaziri tofauti tofauti ambao kwa namna moja au nyingine wanaingia katika suala hili la mpango wa matumizi bora ya ardhi ikiwemo katika sekta ya Madini, Kilimo, Misitu na Mifugo na kuona ni namna gani wataweza kutenga bajeti ambayo itaweza kuingia katika suala hili la matumizi bora ya ardhi,"alisema Nditi

Dkt. Nindi aliongeza kuwa ripoti hiyo itawezesha suala la upangaji  wa matumizi bora ya ardhi linakuwa suala la kitaifa na kuiwezesha  serikali kupanga bajeti itakayofanya mchakato huo wa upimaji na upangaji wa matumizi
bora kwenda kwa haraka na kufikia vijiji vingi zaidi.

Naye Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka asasi ya kiraia ya  CARE INTERNATIONAL nchini Tanzania, Bi.Mary Ndaro alisema serikali inapaswa kuweka dhamira kisiasa ya kuweka utayari wa kufanya suala la ardhi kuwa ni kipaumbele na kuongeza bajeti ya fedha katika suala la matumizi ya ardhi.
Alisema  asasi za kiraia zipo tayari kufanya kazi na serikali pamoja na Wizara zinazohusika na  suala la matumizi bora ya ardhi na kuhakikisha
mabadiliko yanapatika katika suala hilo
 "Tupo tayari kuungana na serikali katika kuhakikisha suala hili linapewa kipaumbe na kupunguza migogoro inayoendelea kujitokeza kwa sasa ya ardhi hivyo
sisi tupo tayari kuona  serikali inatoa  mwongozo wake kupitia Wizara zinazohusiana na masuala ya ardhi kwa pamoja tuungane na kushikamana katika
kusaidia suala hili linafanikiwa na vijiji vinapangwa na kupimwa kwa matumizi bora ya ardhi," alisema Ndaro.

Pia Bi. Ndaro alisisitiza wananchi kuwa watulivu na kukwepa muingiliano kwani asasi hizi zimejizatiti kusaidia wananchi hivyo rai yangu kwa baadhi ya
asasi za kiraia zinazo penda kusaidia mchakato huu ziapaswa kujitokeza kwa wingi ilikuweza kumaliza shughuli hii kwa haraka zaid kwani tukiiachia serikali
peke yake haitoweza kumaliza sehemu zote kwa wakati kwani inabajeti ambayo ni ndogo
ambayo inaweza kumudu vijiji vitano tu kwa mwaka.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI
KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiLzPczB5g2nAJOI84WCcE3w_DASmlpvcujQrAq3VHJtLobNfOekRisWmcOP9uSI-2I7266fp609GwWJhdafNmTDngYnqqgICkNAMEIpwGFC_9o9jvWkNM_qcSNyGMeqgUN2HdPVIrUCXv/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiLzPczB5g2nAJOI84WCcE3w_DASmlpvcujQrAq3VHJtLobNfOekRisWmcOP9uSI-2I7266fp609GwWJhdafNmTDngYnqqgICkNAMEIpwGFC_9o9jvWkNM_qcSNyGMeqgUN2HdPVIrUCXv/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/kikosi-kazi-chamaliza-kazi-ya-kuandaa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/kikosi-kazi-chamaliza-kazi-ya-kuandaa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy