Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameitaka kampuni ya kuzalisha umeme ya SONGAS, kupitia upya mikataba ya gawio kwa s...
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameitaka kampuni ya kuzalisha umeme ya SONGAS, kupitia upya mikataba ya gawio kwa serikali ili kuhakikisha serikali inapata mgao sawa na Kampuni hiyo na kubadilisha mfumo wa sasa ambapo serikali inapata gawiwo la faida baada ya uzalishaji.
Ni katika ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani alipotembelea katika kampuni ya kuzalisha Umeme ya Songas, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo Dkt. Kalemani akaitaka kampuni hiyo kupitia upya mikataba yao katika gawio na serikali.
Aidha Waziri Dkt kalemani amethibitisha mchango wa serikali katika uchangiaji wa uzalishaji wa sekta ya umeme sanjari na kampuni ya Songas pia lakini akakemea vikali tabia ya kutofautiana kwa mgao baina ya kampuni hiyo na Serikali.
Sebastian Kastuli ni meneja biashara wa kampuni ya Songas ambaye anaahidi kutekeleza maagizo ya Waziri na kupitia upya mikataba yao na serikali.
Aidha Waziri Dkt Kalemani amezitaka kampuni zote za uzalishaji nchini kuacha mara moja tabia ya kuagiza mitambo ya uzalishaji nje ya nchi na badala yake ipatikane hapahapa nchini.
COMMENTS