COSOTA, CMEA KUANZA KULIPA MIRAHABA KWA WANAMUZIKI KUANZA JANUARI MWAKANI

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) Doreen Sinare akielezea umuhimu wa wanamuziki kujisajili kwa...











 Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) Doreen
Sinare akielezea umuhimu wa wanamuziki kujisajili kwao kupitia Kampuni
iliyopewa jukumu la kuendesha zoezi usajili, Copyrights Management East
Africa Limited (CMEA) ilikuweza kupata haki zao kutokana  na kazi zao. 

 Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya CMEA, Abdi Zagar akielezea jinsi ya
mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taarifa za wanamuziki kwenye vituo vya
televisheni na redio kwa ajili ya kutumiwa na Cosota ili kufanya malipo
sahihi kwa wanamuziki na wadau wake.

 Mwanamuziki, Elias Barnaba akitoa maada katika semina hiyo iliyoandaliwa na Cosota na CMEA kwa ajili ya kuwapa elimu wanamuziki na wadau wake kuhusiana na malipo ya mirahaba.
 Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akijibu moja ya maswali katika semina hiyo. Mutahaba aliwahamasisha wanamuziki kujisajili CMEA kwa lengo la kupata haki  kutokana na kazi zao.

 Wanamuziki wa muziki wa dansi, Chalz Baba (wa pili kulia) na Jonico Flower wakifuatilia semina hiyo ambayo iliwapa somo kuhusiana na umuhimu wa kujisajili kupitia kampuni ya CMEA na Cosota ili kufaidika na kazi zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akifafanua jambo kuhusiana
na faida za wanamuziki na wadau wake mara baada ya kujisajili na kuanza
kulipwa fedha zao.

Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na kampuni ya
kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa
Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake
kuanzia mwakani.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare
alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60
kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote
ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya
CMEA.

Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata
asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo
na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema
kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo
itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine
katika taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili
kuhakikisha kila mwanamuziki  anafaidika na kazi yake, watashirikiana na
vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati
ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya
redio.

Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama
hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo
vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.

“Lengo
la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya
kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za
mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa
wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.

Afisa
Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki,
kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine
pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo
zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse
alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha
kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni
na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa
malengo maalum.

“Pia
tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya
uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo
vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya
urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

Alisema kuwa
wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki
zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika
redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili,
kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,”
alisisitiza.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: COSOTA, CMEA KUANZA KULIPA MIRAHABA KWA WANAMUZIKI KUANZA JANUARI MWAKANI
COSOTA, CMEA KUANZA KULIPA MIRAHABA KWA WANAMUZIKI KUANZA JANUARI MWAKANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiGsHMwlZBvIYf__eQD0ZNvOXyG48t_oALYfh9jck0NfgRclE4y1ShRd1lqxB3u6ZxKG9LBY7xHuzX5iW4u7BBwCeX48sMtS0cjdMhF20TfzlO6fUDx1Lq0GDaISAcaOJdywgl6kSEKlKl/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiGsHMwlZBvIYf__eQD0ZNvOXyG48t_oALYfh9jck0NfgRclE4y1ShRd1lqxB3u6ZxKG9LBY7xHuzX5iW4u7BBwCeX48sMtS0cjdMhF20TfzlO6fUDx1Lq0GDaISAcaOJdywgl6kSEKlKl/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2015/12/cosota-cmea-kuanza-kulipa-mirahaba-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/12/cosota-cmea-kuanza-kulipa-mirahaba-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy