Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw. Mwadini Jecha (katikati) akiweka saini kitabu cha wageni Idara ya Uratibu wa Maaf...
Rais
wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw. Mwadini Jecha (katikati)
akiweka saini kitabu cha wageni Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu walipotembelea Idara hiyo na kukabidhi Kadi za Uanachama kwa
Idara hiyo, tarehe 16 Februari, 2017.
Mkurugenzi
wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw.Renatus Mkaruka (wa kwanza
kulia) akizungumza jambo wakati wa zoezi la kukabidhi kadi za Uanachama
wa chama hicho kwa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Februari 16, 2017 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi
Msuya (kulia) akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu
Tanzania kutoka kwa Rais wa Chama hicho Bw. Mwadini Jecha Februari 16,
2017 katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
Mratibu
wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles
Msangi akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania
kutoka kwa Katibu wa chama hicho Bw. Julius Kejo Februari 16, 2017
katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
COMMENTS