MAMA JANETH MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na  maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018


HomeJamii

MAMA JANETH MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo ameongoza maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Dunian...

WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA) ILALA WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA VYAMA VYAO DAR ES SALAAM
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA MEI 13, 2017
WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA WADAU WA KOROSHO


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli leo ameongoza maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani huku akiziomba asasi za kiraia, na watu binafsi kushirikiana na serikali kuwapatia kinamama mbinu mbalimbali, mafunzo, mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao.

Mama Magufuli pia ameupongeza mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzisha vikundi zaidi ya 400 vya wanawake vinavyojishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo usindikaji mazao, ushonaji, uchoraji na kadhalika, pamoja na kuwa na vikundi vya kukopeshana (VICOBA) vipatavyo 2,748 ambavyo kwa pamoja vina mtaji wa jumla ya shilingi bilioni 10.78.

"Ni imani yangu kuwa kama mikoa yote na taasisi nyingine za kiserikali na kiraia zitaiga mfano wa Dar es salaam katika kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuwashirikisha kwenye shughuli za ujenzi wa viwanda basi tutawawezesha wanawake kiuchumi ikiwemo kushiriki kwenye shughuli za ujenzi wa viwanda", alisema Mama Magufuli amesema kwenye sherehe hizo zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City.
Huku akishangiliwa kwa nguvu, Mama Magufuli amesema japokuwa serikali inajitahidi sana kuweka usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake kisiasa, kiuchumi, elimu na afya, serikali peke yake haiwezi kuzimaliza changamoto zote, hivyo ni lazima wananchi wenyewe washiriki katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Mama Magufuli amewapongeza viongozi wa awamu zote za nchi, ikiwa ni pamoja na kinamama shupavu wa TANU na ASP na baadaye CCM ambao kwa namna moja ama nyingine wameshiriki katika harakati za kumkomboa mwanamke nchini.

"Kutokana na umuhimu wa siku ya leo naomba nitambue mchango wa Mama Maria Nyerere, Mama Fatma Karume, Bibi Titi Mohamed, Mama Sophia Kawawa, Bi. Hadija Jabir, Bi Johari Yusuf Akida, Mwajuma Koja, Bi. Mtumwa Fikirini na wengineo wengi. Hatuna budi kuwapongeza sana akinamama hawa kwa kupigania haki za wanawake nchini" alisema.

Mama Magufuli ametanabahisha kwamba japokuwa vitendo vya unyanyasaji, dhuluma na ukatili dhidi ya wanawake bado vinaendelea kwenye baadhi ya maeneo nchini, Tanzania  imepiga hatua kubwa na ni  miongoni mwa nchi zinazosifika duniani kwa kulinda na kusimamia haki na maslahi ya wanawake.
"Hivyo basi hatuna budi kuwapongeza wote walioshiriki katika kulinda na kutetea haki na maslahi ya wanawake nchini", alisema, kabla ya kutembelea maonesho ya wajasiriamali kinamama waliopanga bidhaa zao katika kila pembe ya ukumbi huo.
Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda pamoja na wakuu wa Wilaya za Kinodnoni na Ilala, Mhe. Kisare Makori na Bi. Sophia Mjema. 

Wengine ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila pamoja na maafisa  watendaji wa wilaya ya Ubungo.



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala ya wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea tuzo maalumu kutoka kwa  wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kwa mchango wake wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018

 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika kucheza na kuimba nyimbo za hamasa na wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubua maelfu ya wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018





Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori baada ya kuhutubua wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018. Katikati ni  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wengine  katika picha ya pamoja na wawakilisji wa wajasiriamali wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Machi 8, 2018. (PICHA NA IKULU)




 





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAMA JANETH MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
MAMA JANETH MAGUFULI MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjovDF4BfoOo2RzDjDLR9ha69Dv8qibqU8lovCZZ36c3wTG0H1YhFDrVd19ZwJNbjcktbeWrC1BCUpgVUnnWFLqbqVZOGVcma3cEKhaY_h_M2X61f9f7lDhVhg3EhlzuL5o2HqE29GQ5Sk/s640/m+%25281%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjovDF4BfoOo2RzDjDLR9ha69Dv8qibqU8lovCZZ36c3wTG0H1YhFDrVd19ZwJNbjcktbeWrC1BCUpgVUnnWFLqbqVZOGVcma3cEKhaY_h_M2X61f9f7lDhVhg3EhlzuL5o2HqE29GQ5Sk/s72-c/m+%25281%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mama-janeth-magufuli-mgeni-rasmi-katika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mama-janeth-magufuli-mgeni-rasmi-katika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy