TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA
HomeJamii

TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Pr...





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Rais wa Msumbiji Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliopo Havana Cuba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Afrika yaliyopo Havana Cuba.

……………………………………………………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.

Alisema wananchi wa Cuba pamoja na watu kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika wanakwenda katika eneo hilo la makumbusho na kujifunza historia za viongozi hao. Pia eneo hilo linatumiwa na watafiti wa masuala ya kihistoria.

Mashujaa ambao tayari sanamu zao zimekwishawekwa kwenye eneo la kuzunguka mnara huo ni pamoja na Jomo Kenyatta (Rais wa kwanza wa Kenya), Modibo Keita (Rais wa Mali), Amilcar Cabral (Rais wa kwanza wa Guinea Bissau).

Wengine ni Dkt. Kwame Nkrumah (Rais wa kwanza Ghana), Oliver Thambo (Kiongozi Mwandamizi wa Chama cha Ukombozi cha ANC cha Afrika Kusini), Eduardo Chivambo Mondlane (Kiongozi wa ukombozi nchini Msumbuji).

Wengine ni Samora Moises Machel (Rais wa kwanza wa Msumbuji), Sekou Toure (Rais wa kwanza wa Senegal), Seretse Khama (Rais wa kwanza wa Botswana), Alhaji Aboubakar Tafawa Balewa na Obafemi Jeremiah Awolowo (Mawaziri Wakuu wa zamani wa Nigeria) na Chifu Jeremia Azikiwe (Rais wa zamani wa Nigeria) .
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA
TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgf6iyKSJUQgnd_WG7PGpNNScPHhuMXdMZYseA9LMehbdtKnusiFNhJxSXu1tYZhwFmEMffZvdhehG4-NISCinxxOaQHRvu8eWNHQeoZCG8KTk2O5k-94EzwKUBkrAPhG5q6Tq5DWhFvag/s640/PMO_0015.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgf6iyKSJUQgnd_WG7PGpNNScPHhuMXdMZYseA9LMehbdtKnusiFNhJxSXu1tYZhwFmEMffZvdhehG4-NISCinxxOaQHRvu8eWNHQeoZCG8KTk2O5k-94EzwKUBkrAPhG5q6Tq5DWhFvag/s72-c/PMO_0015.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tunaishukuru-serikali-ya-cuba-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/tunaishukuru-serikali-ya-cuba-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy