Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing ofisini kwak...
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na
balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing ofisini kwake leo mjini Dodoma
ambapo wamejadili na kukubaliana mambo mbali mbali ya kuimarisha
uhusiano wa China na Tanzania katika sekta ya maliasili na utalii.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwakaribisha wawekezaji katika
sekta ya viwanda vya uchakataji wa mazao ya misitu na ujenzi wa hoteli
katika fukwe za Tanzania na Hifadhi za Taifa.
Balozi
wa China nchini, Dkt. LU Youqing akimueleza jambo Waziri wa Maliasili
na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini
Dodoma leo. Balozi huyo amekubali ombi la Waziri Maghembe kuwaleta wadau
wa mashirika ya utalii kutoka nchini China kwa ajili ya kutembelea
vivutio vya utalii vya Tanzania na kuvitangaza nchi kwao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing baada ya mazungumzo marefu ofisini kwake leo mjini Dodoma.
COMMENTS