MTANZANIA ATEULIWA NAIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA MAZINGIRA
HomeJamii

MTANZANIA ATEULIWA NAIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA MAZINGIRA

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Joyce Msuya kutoka Tanzania kuw...

SHEREHE ZA MIAKA 56 YA UHURU MJINI DODOMA LEO
THBUB YAMPONGEZA RAIS KUWAFUTIA WATU 61 ADHABU YA KIFO
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA MHE. SPIKA KWA WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI


Na Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Joyce Msuya kutoka Tanzania kuwa naibu katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia program ya mazingira yenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa mataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 22 Mei, Msuya anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Ibrahim Thiaw wa Mauritania aliyemaliza muda wake ambaye katibu Mkuu wa umoja wa mataifa amemuelezea kuwa na utumishi uliotukuka katika kipindi chake cha uongozi.

Bi Msuya amekua akifanya kazi kama mshauri wa makamu wa rais wa benki ya dunia anayeshughulikia nchi za Asia Mashariki pamoja na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2017, makao makuu ya benki ya Dunia Washington D.C Marekani.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Msuya atatumia muzoefu wake wa miaka 20 katika benki ya Dunia, pamoja na uzoefu wake katika masuala ya maendeleo ya kimataifa katika kazi yake mpya na anaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa katika umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bi.Msuya amewahi kufanya kazi kama mwakilishi maalum wa benki ya Dunia na mkuu wa kundi la benki ya dunia nchini Korea ya kusini,pamoja na mratibu wa taasisi ya benki ya dunia katika Asia Mashariki na ukanda wa Pasifiki ofisi iliyoko China, na ameahi kuwa na nafasi mbalimbali za juu katika benki ya dunia na washirika wake.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa, Joyce Msuya ana Shahada ya uzamili ya Maikrobailojia na kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada pamoja na shahada ya Baiokemia kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde,Scotland.

Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira ni mpango wa kidunia wa mazingira unaolenga kutoa mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa mazingira, na kuwashauri wadau na nchi wanachama kwa ujumla njia sahihi za kutunza na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira inafanya kazi na serikali, mashirika na asasi za kimataifa duniani kote. 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MTANZANIA ATEULIWA NAIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA MAZINGIRA
MTANZANIA ATEULIWA NAIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA MAZINGIRA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgctTOlquSptVsHr8-n-U09_ssD6SijhsGFOsl6fWj6v2jn8W5o_CFeoXHstHWhyuSev3X4wUtZ-_cPbG7JaSy-1SMbYpIBmAhojB6Xmo4Jkwi-qMjDezIOvEcdM7ut3nsGqwHfdEkVtI_7/s400/Ms.+Msuya-photo.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgctTOlquSptVsHr8-n-U09_ssD6SijhsGFOsl6fWj6v2jn8W5o_CFeoXHstHWhyuSev3X4wUtZ-_cPbG7JaSy-1SMbYpIBmAhojB6Xmo4Jkwi-qMjDezIOvEcdM7ut3nsGqwHfdEkVtI_7/s72-c/Ms.+Msuya-photo.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/05/mtanzania-ateuliwa-naibu-katibu-mkuu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/05/mtanzania-ateuliwa-naibu-katibu-mkuu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy