THBUB YAMPONGEZA RAIS KUWAFUTIA WATU 61 ADHABU YA KIFO
HomeJamii

THBUB YAMPONGEZA RAIS KUWAFUTIA WATU 61 ADHABU YA KIFO

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 21...




-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz

Desemba 9, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

THBUB yampongeza Rais kwa kuwafutia watu 61 adhabu ya kifo

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga kwa niaba ya Tume na Wafanyakazi wote wa THBUB anachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wake wa kufuta adhabu ya kifo kwa watu 61 waliokuwa magereza mbalimbali nchini, wakisubiri utekelezaji wa adhabu ya kifo dhidi yao.

Tume inampongeza sana Mhe. Rais kwa uamuzi wake huo kwani unaendana na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Na. 62/149 la tarehe 18 Desemba 2007 linalozitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kufuta au kusimamisha utekelezaji wa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala.

Tume inatambua kwamba, kama alivyosema Mhe. Rais, msamaha huu haufuti adhabu ya kifo katika sheria za nchini.

Hivyo, kutokana na mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 130(1) (g), Tume inapenda kuchukua nafasi hii kuishauri Serikali kuona uwezekano wa kufuta adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala, ili iendane na Azimio la Umoja wa Mataifa  lililotajwa hapo juu.

Pia, Tume inaisihi Serikali, hususan Idara yake ya Ustawi wa Jamii kuwasaidia, na Wananchi kwa ujumla kuwapokea, wale wote waliopewa msamaha ili waweza kuendelea na maisha yao kama raia wema katika jamii.

Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Desemba 9, 2017

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: THBUB YAMPONGEZA RAIS KUWAFUTIA WATU 61 ADHABU YA KIFO
THBUB YAMPONGEZA RAIS KUWAFUTIA WATU 61 ADHABU YA KIFO
https://lh5.googleusercontent.com/9EHodxXyIINFtQ8Ww3k1qKa7l3h9UcqBA0dl5fiZpnfgvxfCMS5gFLHvNB6WtVrbpFqGVfcHLpVE9tCSULbO27qD-WLVn_xbsQZwhxAG-yAudAV3g86xnUWgmrKH_dmil9f8uL-6IMGrWe3pGg
https://lh5.googleusercontent.com/9EHodxXyIINFtQ8Ww3k1qKa7l3h9UcqBA0dl5fiZpnfgvxfCMS5gFLHvNB6WtVrbpFqGVfcHLpVE9tCSULbO27qD-WLVn_xbsQZwhxAG-yAudAV3g86xnUWgmrKH_dmil9f8uL-6IMGrWe3pGg=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/thbub-yampongeza-rais-kuwafutia-watu-61.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/thbub-yampongeza-rais-kuwafutia-watu-61.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy