JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA Simu: +255 022 2112065-7 Fax No. +255 022 2112538 E-mail: info@bunge.go.tz...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIABUNGE LA TANZANIA | ||
Simu: +255 022 2112065-7
Fax No. +255 022 2112538
E-mail: info@bunge.go.tz |
Ofisi ya Bunge,
S.L.P. 941,
DODOMA |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewatumia salamu za Rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo kufuatia kuuawa kwa Askari 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopo katika operesheni ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa hizi za kuuawa kwa Askari wetu waliokuwa wanalinda amani huko DRC, hakika hili ni pigo kwa Taifa zima, naungana na Watanzania wenzangu kuwapa pole kwa msiba huu mzito, ninamuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za wapendwa wetu mahala pema peponi,” Alisema Mhe. Ndugai.
“Natoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza wapendwa wao, Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” aliongeza Mheshimiwa Ndugai.
Vilevile, Mheshimiwa Spika pia amewaombea Askari 44 waliojeruhiwa wapone haraka ili waweze kurejea katika majukumu yao na pia Askari 2 waliopotea waweze kupatikana wakiwa salama.
Imetolewa na: Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA
09 Desemba, 2017.
COMMENTS