ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA YAWA NA MAFANIKIO UKEREWE
HomeJamii

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA YAWA NA MAFANIKIO UKEREWE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili Nansio wilayani Ukerewe kwa meli ya MV. Nyehun...

UJUMBE WA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUHUSU MADINI
SPIKA NDUGAI ATEMBELEA BUNGE LA KENYA
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TAMISEMI




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili Nansio wilayani Ukerewe kwa meli ya MV. Nyehunge II ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi wa  Nansio wilayani Ukerewe waliojitokeza kumpokea ambapo aliwasili kutokea Mwanza mjini kwa meli ya MV. Nyehunge II ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi mbali mbali katika kukagua  mradi mkubwa wa maji wa Nebuye
wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Nebuye ambapo aliwasihi kuutunza mradi wa maji na mazingira kwa ujumla wakati wa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji ya Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisoma maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wa
Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwapungia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wakati akiwasili tayari kuhutubia wakazi wa kijiji hicho.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe na kusisitiza serikali ya awamu ya tano ni ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Tanzania.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kutaka kumsalimia na kuwakilisha kero zao wakati wa ziara yake katika wilaya ya Ukerewe



                                         .................................................................. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.

Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika Ziwa Victoria kwenda kisiwa Ukerewe kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo, amewahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.


Mradi huo ambao unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano unamikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji. 


Akihutubia mamia ya wananchi  wa kisiwa cha ukerewe kwenye kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais amewapa pole wananchi wa kisiwa hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba 2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA YAWA NA MAFANIKIO UKEREWE
ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA YAWA NA MAFANIKIO UKEREWE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhp02t-j9u4noUr-yNcfkRq0QmJXFXJD2zUM1BaDB8d1tD2v_halwOmMCkVnTqyQ39c4Df-v3Adbk0G-Ehudyrbhn4mXxyDCx4L0DifNC_IWnfp-RO0IbxS5wFFwualr4zAe7Z6GnV_n4/s640/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhp02t-j9u4noUr-yNcfkRq0QmJXFXJD2zUM1BaDB8d1tD2v_halwOmMCkVnTqyQ39c4Df-v3Adbk0G-Ehudyrbhn4mXxyDCx4L0DifNC_IWnfp-RO0IbxS5wFFwualr4zAe7Z6GnV_n4/s72-c/2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/ziara-ya-makamu-wa-rais-mhesamia-yawa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/ziara-ya-makamu-wa-rais-mhesamia-yawa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy