NAIBU WAZIRI WA UJENZI by Anonymous zPUXs8aO on Scribd Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akifungua mkutano Uliowakutanish...
 |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akifungua mkutano Uliowakutanisha Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Menejimenti ya Sekta Mawasiliano (hawapo pichani), kujadili namna ya kuzingatia sheria za manunuzi Mkoani Dodoma.Kulia ni Afisa Utumishi Mwandamizi wa Sekta ya Mawasiliano, Trano Mubarok.
|
 |
Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Marwa Chacha, akimwoyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, baadhi ya vifaa vilivyotengenezwa kwenye moja ya magari ya Serikali yanayotengezwa na Wakala huo, wakati Naibu Waziri huyo alipokagua karakana ya magari ya wakala huo Mkoani Dodoma.
|
 |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akiangalia uchakavu wa moja ya nyumba zinazomilikiwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), alipokagua nyumba hizo Mkoani Dodoma. TBA mpaka sasa inamiliki nyumba zaidi ya 800 mkoani humo.
|
 |
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Steven Simba (kulia), akimweleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), hatua iliyofikiwa ya ukarabati wa moja ya nyumba za viongozi, wakati Naibu Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ukarabati wa nyuma za viongozi Mkoani Dodoma.
|
 |
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (wa kwanza), akitoa maelekezo kwa Uongoz wa Wakala wa MAjengo Nchini (TBA), alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkoani Dodoma.
|
COMMENTS