WANAKIJIJI WALIO KWENYE MRADI WA BACKBONE KUUNGANISHIWA UMEME KWA SHILINGI 27,000
HomeJamii

WANAKIJIJI WALIO KWENYE MRADI WA BACKBONE KUUNGANISHIWA UMEME KWA SHILINGI 27,000

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida WANAKIJIJI wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa...

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI WA HAMSINI NA MOJA WA SEKTA ZA AFYA NA KILIMO WAAPISHWA LEO
HIVI NDIVYO INTANETI INAVYOATHIRI MAISHA YAKO YA KILA SIKU
UTALII WA BALOON WAWA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENETI.















NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
WANAKIJIJI wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga
kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi.
Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.
Bi Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.
“Nia ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema,
Kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme, TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei
nafuu.” Aliongeza.
 Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga
hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.
Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza
umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa
Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.
Mradi huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu
shilingi Trilioni 1. Kazi iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme, vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua.


 Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, akizungumza kwenye kituo cha Kibaoni Singida.

 Mkuu wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kibaoni mkoani Singida, akitoa maelezo kwa wahariri.


 Mhariri wa Star TV, Jenifer Sumi.
 Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akinakili maelezo ya kiufundi kuhusiana na kituo cha umeme cha Kibaoni mkoani Singida.
 Picha ya pamoja ya wahariri na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Singida.
 Kituo cha Kibaoni mkoani Singida ambacho kilifanyiwa upanuzi chini ya mradi wa Backbone.

 Mdhibiti mifumo ya umeme kituo cha Kibaoni Mkoani Singida, aimuonyesha kitu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), Neville Meena
 Minara ya kubeba nyaya za kusafirisha umeme, upande wa kulia ni minara mipya na kushoto ni ile ya zamani.


 Mhariri wa Star TV, Jenifer Sumi.

 Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akinakili maelezo ya kiufundi kuhusiana na kituo cha umeme cha Kibaoni mkoani Singida.
 Picha ya pamoja ya wahariri na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Singida.

 Kituo cha Kibaoni mkoani Singida ambacho kilifanyiwa upanuzi chini ya mradi wa Backbone.

 Mdhibiti mifumo ya umeme kituo cha Kibaoni Mkoani Singida, aimuonyesha kitu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), Neville Meena.

 Minara ya kubeba nyaya za kusafirisha umeme, upande wa kulia ni minara mipya na kushoto ni ile ya zamani.


Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WANAKIJIJI WALIO KWENYE MRADI WA BACKBONE KUUNGANISHIWA UMEME KWA SHILINGI 27,000
WANAKIJIJI WALIO KWENYE MRADI WA BACKBONE KUUNGANISHIWA UMEME KWA SHILINGI 27,000
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAYApN6TBhx4HNE3omTXHlEIOGskFpLMmA0UvDSY6jRFUedTRCt2acRv3NNWLZupWgSsv6VHqffpjNcyy-_v4RqaFke0Qvwkk3ln2ZOucFD5F8knRvgjV5TxKqodJRwV5l6Qg4Empef8w/s640/5R5A9671.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAYApN6TBhx4HNE3omTXHlEIOGskFpLMmA0UvDSY6jRFUedTRCt2acRv3NNWLZupWgSsv6VHqffpjNcyy-_v4RqaFke0Qvwkk3ln2ZOucFD5F8knRvgjV5TxKqodJRwV5l6Qg4Empef8w/s72-c/5R5A9671.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wanakijiji-walio-kwenye-mradi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/wanakijiji-walio-kwenye-mradi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy