MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI
HomeJamii

MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa w aziri wa mambo ya ...

BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO
SEKTA BINAFSI YACHANGIA MAADALIZI YA WIKI YA TANZANIA NA NCHI YA KENYA
TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA (TEWW) KUENDELEA KUWA KITOVU CHA KUTOA ELIMU BORA.



Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo.
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.



Na Fredy Mgunda,Dodoma.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amelibana jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo

Mbunge Rose Tweve mapema hii leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo.

Akijibu swali la mbunge Rose Twelve, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba alisema kuwa jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani limeweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 43 kwa mwaka 2017

Dkt. Mwigulu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856 ambazo zilisababisha vifo 3256 na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017 kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo 2533 na majeruhi 5355.

Waziri Mwigulu ameongeza kuwa kwa kipindi cha januari hadi februari 2018 kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo 334 na majeruhi 698.

Akiuliza swali la nyongeza mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda wahanga wa ajali hizo, sasa mheshimu waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha wanamapungufu mengi na watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo na kwanini tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.

Akijibia swali la Nyongeza la Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia, Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa ajali 1583 wakilipwa fidia takribani Bilioni  7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.

Katika hatua nyingine Dkt. Nchemba amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500 yanayosababishwa na uzembe wa madereva
huku serikali ikipanga kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.

“Ni kweli serikali itahakikisha inawachukulia hatua madereva wazembe ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili kupunguza idadi ya madereva ambao wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuepkukika” alisema Mwigulu nchemba.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI
MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2Kf5zTD7ZD_XXvMYMS122UjBXwXEo7WDzv8BLoCcTjv-wRbPJvYmMtmGaw0FiUwbLDSR25kD1qP8-w5r017TwFsqy6OBkE5Au3o-OgQA8MgbQFcPGKUwSAhqrl7sKLfDgo6pIaPktHI2Y/s640/IMG-20180403-WA0174.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2Kf5zTD7ZD_XXvMYMS122UjBXwXEo7WDzv8BLoCcTjv-wRbPJvYmMtmGaw0FiUwbLDSR25kD1qP8-w5r017TwFsqy6OBkE5Au3o-OgQA8MgbQFcPGKUwSAhqrl7sKLfDgo6pIaPktHI2Y/s72-c/IMG-20180403-WA0174.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mbunge-rose-tweve-ambana-waziri-mwigulu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/mbunge-rose-tweve-ambana-waziri-mwigulu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy