SEKTA BINAFSI YACHANGIA MAADALIZI YA WIKI YA TANZANIA NA NCHI YA KENYA
HomeJamii

SEKTA BINAFSI YACHANGIA MAADALIZI YA WIKI YA TANZANIA NA NCHI YA KENYA

Serikali itadumisha ushirikiano na sekta binafsi katika kutafuta fursa za kibiashara katika soko la pamoja la Afrika Mashariki na ma...

FAO NA USAID TANZANIA WAIPIGA TAFU SERIKALI KUKINGA KICHAA CHA MBWA
WAZIRI KAIRUKI AZINDUA RIPOTI YA NANE YA TEITI
WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI MJINI IRINGA



Serikali itadumisha ushirikiano na sekta binafsi katika kutafuta fursa za kibiashara katika soko la pamoja la Afrika Mashariki na maeneo mengine duniani ili kujenga uchumi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakati akipokea michango ya wadau toka sekta binafsi kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya wiki ya Tanzania nchini Kenya.
"Ninawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na kuonyesha uthubutu wa kuingia katika soko la Kenya, ninyi ni mabalozi wa wafanyabiashara wengine katika kutafuta fursa za kibiashara nje ya Tanzania"alisema Balozi Mahiga.
Balozi Mahiga alisema Tanzania inazobidhaa nyingi za viwanda ambazo nchi nyingine hawazijui bidhaa hizo, hivyo kinachofanywa na sekta binafsi kushirikiana na Serikali jambo la kijivunia.
Aidha, Balozi Mahiga alisema kuwa kufanya biashara nje ya nchi kunaimarisha uhusiano wa kisiasa baina ya Serikali ya Tanzania na nchi nyingine na kukuza diplomasia ya uchumi.Aliongeza kuwa hii ni fursa kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ambao ni msisitizo na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Waliotoa michango yao ni Kampuni ya Konyagi ambao wamechangia shilingi milioni 11, Mohamed Enterprises, Shilingi milioni 25 na NIDA TEXTILE MILLS (T) LTD imetoa hundi ya shilingi milioni 22.
Balozi Mahiga amewaomba wafanyabiashara wengine wajitokeze kuchangia na kushiriki katika fursa hiyo ya kutafuta masoko nje ya nchi hususan Kenya ambapo bidhaa za Tanzania zitaoneshwa huko kuanzia tarehe 25 hadi 28, Aprili, 2018.
Kwa upande wake, mwakilishi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Rehema Mtingwa, amesema sekta binafsi iko tayari kushirikiana na Serikali katika kufanikisha upatikanaji wa fursa za kibiashara nchini Kenya na sehemu nyingine.
Hii ni mara ya pili kwa wadau toka sekta binafsi kuchangia maandalizi hayo, kundi la kwanza ambalo lilijumuisha KNAUF Company LTD, IPP Media, Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Bravo Logistics na Lake Oil Company Limited, liliwasilisha michango yake juma lililopita.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SEKTA BINAFSI YACHANGIA MAADALIZI YA WIKI YA TANZANIA NA NCHI YA KENYA
SEKTA BINAFSI YACHANGIA MAADALIZI YA WIKI YA TANZANIA NA NCHI YA KENYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpCsoa4QQFTyhg7DEdFssRlE5k4ght5HWQAd2DDpm6wPoSggz8F9Y3M_okJO5ut545cORUBeDTFgfh-ZVDZJvP8cgyDI1oK0m2GFnDztqzRNhGhlFL3cPfvZ02asglUZb6m-gRzXaQxr66/s400/Waziri-Mahiga.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpCsoa4QQFTyhg7DEdFssRlE5k4ght5HWQAd2DDpm6wPoSggz8F9Y3M_okJO5ut545cORUBeDTFgfh-ZVDZJvP8cgyDI1oK0m2GFnDztqzRNhGhlFL3cPfvZ02asglUZb6m-gRzXaQxr66/s72-c/Waziri-Mahiga.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/sekta-binafsi-yachangia-maadalizi-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/sekta-binafsi-yachangia-maadalizi-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy