Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwak...
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Jamhuri ya
Watu wa China zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 70 kutoka kwa Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing iliyotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya ya Wachina wanaoishi Tanzania kuchangia shule ya msingi ya Chato iliyopo mkoani Geita wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa pamoja na wasanii waliotumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Sehemuya watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
.........................................................................................
PICHA ZA ZIADA NIME ATTACH

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania
itaendelea kudumisha,kuimarisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania
na China kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo MBILI.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina hapa
nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa China na Tanzania.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na mdau mkubwa
wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano mema na mazuri
yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.
Makamu wa
Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing kuwa serikali ya
awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya China hasa katika uimarishaji
wa sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na
ustawi wa wananchi wa Tanzania na China.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi kutoka China
ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana na Taifa la China kupiga
hatua kubwa ya kimaendeleo.
Amehimiza ubadilishanaji
wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali kama hatua ya
kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.
Kwa Upande wake, Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu
Youqing amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana
na rushwa na ufisadi.
Dkt Lu Youqing amesema serikali ya China na raia
wake wanafurahishwa na hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa
na ufisadi kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha
utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.
Akizungumzia
mwaka mpya wa Kichina hapa nchini Balozi huyo amesema maadhimisho hayo ni
muhimu kwa sababu raia Wachina na Tanzania wanajumuika pamoja katika kubadilisha
mawazo na kutakiana heri na mafanikio kwa mwaka 2017.
Balozi huyo
wa Tanzania hapa nchini Dkt Lu Youqing pia
amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi
Moja katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo
inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma asili kutoka
China na maonyesho.
Katika Maadhimisho
hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt Lu Youqing amemkabidhi Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika
katika ujenzi kwenye shule ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.PICHA ZA ZIADA NIME ATTACH
COMMENTS