Na Mwandishi Wetu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016...
Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu,
Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa
kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa
hivi karibuni.
Serikali imetenga
Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao,
wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa
kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata
mikopo.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw.
Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online
Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi
Januari 31, 2017.
“Wanachotakiwa
kufanya wanafunzi ni kuingia katika
mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa
Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa
barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.
Bw.
Badru, katika taarifa yake inayopatikana pia katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ameongeza kuwa Bodi
haitapokea wala kuzifanyia kazi fomu za rufaa ambazo zitawasilishwa Bodi na
wanafunzi bila kupitia kwa maaifsa mikopo wa vyuo vyao.
COMMENTS