BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo.
HomeJamii

BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sr...

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA MPANGO WA ELIMU YA RUSHWA KUTUMIA MABASI YA UDART LEO
WAZIRI MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR
WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WACUBA KUJENGA VIWANDA TANZANIA





Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (wa pili kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo na viongzi wengine baada ya Hati za Utambulisho.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) ambaye anawakilisha pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka akipongezwa baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Maithripala SIRISENA, Rais wa nchi hiyo.

Aprili 12 2018, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Maithripala SIRISENA.

Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza, kuimarisha na kukuza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Sri Lanka ambao ulianza mnamo miaka ya tisini. Wakati huo, Sri Lanka ilikuwa inawakilishwa nchini Tanzania kupitia Ubalozi wake wa mjini Kampala, Uganda ambao baadaye ulifungwa na Tanzania ikiwakilishwa nchini Sri Lanka kupitia Ubalozi wake wa New Delhi. Kwa sasa Sri Lanka inakusudia kumteua Balozi wake mjini Nairobi ambaye pia ataiwakilisha nchi hiyo nchini Tanzania.

Katika hafla hiyo, Balozi Luvanda aliambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania nchini India, Col. Amri Salim Mwami. Aidha, Balozi Luvanda alifanya mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Sri Lanka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Afrika, ambapo ameahidi kushirikiana kwa karibu na watendaji hao katika kudumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili na ambao utazinufaisha zaidi, hususan katika kuhakikisha uhaulishaji wa uzoefu, teknolojia na utaalam wa Sri Lanka kwa Tanzania kwenye sekta ya viwanda vya nguo, madini na vito mbali mbali na kilimo.

Sri Lanka ni nchi yenye uchumi unaoendelea ingawa imepitia kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa takriban miaka 25, vita ambavyo vilimalizika mwaka 2009.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO
BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmjYyWrfJyshVqJkCXKxZcDjLUUTcACfGmZ4r1IETNiiiQQtYqNSenNTLHX1etK6N3oHqGk6vu1nD4cXzG12q_yhDKMLXcresXKUH6-K1M1SpbmYMu1j0iJoOkc2ZpX5jC5UxLHFNe5Qw/s640/LUVANDA2.webp
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmjYyWrfJyshVqJkCXKxZcDjLUUTcACfGmZ4r1IETNiiiQQtYqNSenNTLHX1etK6N3oHqGk6vu1nD4cXzG12q_yhDKMLXcresXKUH6-K1M1SpbmYMu1j0iJoOkc2ZpX5jC5UxLHFNe5Qw/s72-c/LUVANDA2.webp
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/balozi-wa-tanzania-nchini-sri-lanka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/balozi-wa-tanzania-nchini-sri-lanka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy