MHE.MGALU AWASHA UMEME KITUO CHA GONGOLAMBOTO DAR ES SALAAM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyekaa) akiwasha umeme katika kituo cha Gongolamboto kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya Kompyuta. (Picha na Zuena Msuya)

HomeJamii

MHE.MGALU AWASHA UMEME KITUO CHA GONGOLAMBOTO DAR ES SALAAM

Na Zuena Msuya, Dar es Salaam Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolam...

KAMPUNI YA TATU MZUKA NA NAIBU WAZIRI MAVUNDE WAKABIDHI MATOFALI 3000 NA MIFUKO YA SARUJI 100 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI MPYA ZA MBANDE NA MUUNGANO MKOANI DODOMA
HESLB YATANGAZA WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WALIOPATA MIKOPO
WANAFUNZI WA FEZA WASHIRIKI MAONENSHO YA SAYANSI JIJINI DAR ES SALAAM

Na Zuena Msuya, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolamboto chenye uwezo wa MVA 65 na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mgalu alisema Kituo hicho  kinapokea umeme  kutoka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi katika line ya 132 kV.
Mgalu alifafanua kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumewezesha uboreshaji wa upatikanaji wa umeme  katika maeneo ya Kurasini, Kipawa, Kitunda, Chanika na Kisarawe,  Ubungo, Mbagala na GongolaMboto.
“Kwa sasa hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yakisambaziwa umeme kutoka katika kituo hiki haitakuwepo tena, hivyo Serikali itaendelea na juhudi kuwasha umeme katika vituo vingine vilivyosalia,” alisisitiza Mgalu.
Kituo cha Gongolamboto ni miongoni mwa vituo 19 vya kupoza na kusambaza umeme nchini vilivyo katika mradi wa uboreshaji wa vituo hivyo unaofadhiliwa na TEDAP  ambapo Jiji la Dar es salaam lina vituo 11,  Arusha vituo Sita (6) na Kilimanjaro vituo viwili (2).


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya uendeshaji wa kituo cha Gongolamboto , kutoka kwa  Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James,(mbele)  wakati akikagua mitambo ya kituo hicho kabla ya kuwasha kwa mtambo huo.kushoto ni Kaimu Meneja Miradi , Mhandisi Emmanuel Manirabona.

Baadhi ya watendaji katika kituo cha Gongolamboto, wakikamilisha kazi kabla ya kuwasha umeme katika  kituo hicho.


Transfoma iliyofungwa mwaka 57, (kulia) iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza umeme katika kituo cha Gongolamboto,na mpya zilizowekwa sasa (kushoto).

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akionyeshwa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa umeme katika kituo cha Gongolamboto jijini Dar es salaam na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James (katikati) na Kaimu Meneja Miradi, Mhandisi Emmanuel Manirabona.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akizungumza na mkandarasi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala. kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James. (Imeandaliwa na Robert Okanda)





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHE.MGALU AWASHA UMEME KITUO CHA GONGOLAMBOTO DAR ES SALAAM
MHE.MGALU AWASHA UMEME KITUO CHA GONGOLAMBOTO DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh766JfFZ36MURels2iA4CZbDch247GZPHG1VdSeGwHcLbpU2-QNnPJb8AyTGh60tlSANPN09xAFeC6FnV33-IVuM_agTeIFIN39ygDy_FqUOKfjZpI0jjQi_yjLOt6rLSQlrewmQUhbgY/s640/picha+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh766JfFZ36MURels2iA4CZbDch247GZPHG1VdSeGwHcLbpU2-QNnPJb8AyTGh60tlSANPN09xAFeC6FnV33-IVuM_agTeIFIN39ygDy_FqUOKfjZpI0jjQi_yjLOt6rLSQlrewmQUhbgY/s72-c/picha+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mhemgalu-awasha-umeme-kituo-cha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/02/mhemgalu-awasha-umeme-kituo-cha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy