HESLB YATANGAZA WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WALIOPATA MIKOPO
HomeJamii

HESLB YATANGAZA WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WALIOPATA MIKOPO

ยท           Yafungua dirisha la rufaa hadi Novemba 19 Na Mwandishi Wetu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) im...





ยท         Yafungua dirisha la rufaa hadi Novemba 19
Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha nyingine yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353.
Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481), Awamu ya Tatu (7,901).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumapili, Novemba 12, 2017) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, orodha kamili ya wanafunzi hao inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na pia imetumwa kwa vyuo husika leo ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.
โ€œTumekua tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea, na kila tunapokamilisha, tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa mikopo ambao wana sifa โ€“ leo tumetoa hao 1,775,โ€ amesema Bw. Badru.
Bw. Badru, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari pia amekumbusha kuwa kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.
Fedha hizo, shilingi 427.54, ni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi 122,623 wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea na masomo.
Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa
Wakati huohuo, HESLB imetangaza kufungua dirisha la rufaa kuanzia leo, Jumatatu, Novemba 13, 2017 hadi Novemba 19, 2017 ili kuwapa fursa waombaji wote ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa HESLB, lengo la HESLB ni kuhakikisha wanatangaza orodha ya majina ya waombaji mikopo waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo au kabla ya tarehe 30 Novemba mwaka huu.
โ€œTunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafuzi na kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo kabla ya Novemba 22, 2017 ili kuiwezesha Bodi kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba 30, 2017,โ€ amesema Bw. Badru katika taarifa yake.
Maelezo ya kina kuhusu utaratibu wa kuwasilisha rufaa yatatolewa kupitia tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). 

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HESLB YATANGAZA WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WALIOPATA MIKOPO
HESLB YATANGAZA WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WALIOPATA MIKOPO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh2rnI208AAcaGwz0WTras2YglIqtNid5Y9z43hPqEzxLm0RfGUWSOqhNC0v5Phqea5w3jrZqFK98qa2ScAmlQnKgBHQX6keNLVSRADtFN3YSJQ3jgQI4Y31RTdl_aD0C5lzdgi20F5eg/s400/HELSB+LOG.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh2rnI208AAcaGwz0WTras2YglIqtNid5Y9z43hPqEzxLm0RfGUWSOqhNC0v5Phqea5w3jrZqFK98qa2ScAmlQnKgBHQX6keNLVSRADtFN3YSJQ3jgQI4Y31RTdl_aD0C5lzdgi20F5eg/s72-c/HELSB+LOG.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/heslb-yatangaza-wengine-1775-wa-mwaka.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/heslb-yatangaza-wengine-1775-wa-mwaka.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy