Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), inamlilia kwa masikitiko makubwa Mwanasheria wake marehemu Bi. Delfine Mu...
Na
Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), inamlilia kwa masikitiko makubwa Mwanasheria
wake marehemu Bi. Delfine Mulogo (32) aliyekuwa Kituo cha kazi cha Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) aliyefariki tarehe Desemba 25.
Mkuu
wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Bw. Mtengela Hanga akisoma wasifu wa marehemu
katika kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustine Mbezi Temboni, alisema
atakumbukwa kwa uchapakazi, uhodari na uadilifu wake kazini.
“Tunasikitika
kumpoteza mwanasheria huyu kijana, kwa niaba ya Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania, tunatoa pole kwa wafiwa kwa kuondokewa na mpendwa
wao, lakini sisi kama mamlaka na taifa kwa ujumla tumempoteza mtu muhimu sana aliyekuwa
mchapakazi, tutamkumbuka sana marehemu,” alisema Bw. Hanga.
Marehemu
ambaye ameacha mume Bw. Alex Temba na watoto wawili Faith Temba (9) na Harieth
Temba (4) alihamishiwa TAA tarehe 01/04/2016 akitokea Halmashauri ya Manispaa ya
mji wa Songea alipokuwa akifanya kazi kama mwanasheria kuanzia mwaka 2012.
Naye
Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Bw. Stephen Msechu alisema
marehemu alikuwa mwanachama tangu alipoapishwa kuwa Wakili mwaka 2012 na kupewa
namba ya uanachama 3361 na amekuwa akishirikiana nao katika shughuli mbalimbali
kwa uadilifu mkubwa.
Hata
hivyo, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustine lililopo Mbezi Temboni,
Padri Fidelis Mfaranyembo aliwataka waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa
marehemu Delfine kujiandaa wakati wote
kwa kuwa hatujui saa wala siku watakayotwaliwa.
Padri
Mfaranyembo alisema pia waombolezaji wahakikishe wanakuwa watu wa sala wakati
wote ili kumuombea marehemu aweze kupokelewa na aingie katika ufalme wa
mbinguni, kwani ufalme huo upo kwa kuwa kunamaisha baada ya kifo.
“Kuna
mwanafalsafa mmoja wa zamani, Plato alitafakari
sana kuwa mwanadamu akifa anakwenda wapi? na akaona kila mwanadamu anabeba
roho ya muumbaji na hivyo unapokufa roho
inarudi kwa yule aliyeiumba, Plato anatufundisha ya kwamba mwisho wa maisha
yake hapa duniani Mwanadamu anarudi kwa Mungu wake kulingana na namna
alivyokuwa akiishi na wengine hapa duniani,” alisema Padri Mfaranyembo.
Pia
amemtaka mume wa marehemu Bw. Temba asifadhaike kwa kuondokewa na mkewe, bali
ajikabidhi kwa Mungu kwa kumuomba hakika atamsaidia kwa kumtia nguvu na kumpa
uwezo wa kuendelea kuwahudumia watoto wake kwa kadri ya uweza wake Mungu.
Marehemu
alipata elimu ya msingi katika shule ya Oysterbay (1991), baadaye sekondari ya
St. Mathew (1998), na baadaye elimu ya Kidato cha Tano na Sita katika shule ya
Wasichana ya Kibosho (2004), na mwaka 2008 alihitimu Shahada ya Kwanza ya
Sheria katika Chuo Kikuu cha Tumaini.
![]() |
Mwanasheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Kituo cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), marehemu Delfine Mulogo enzi za uhai wake. |
COMMENTS