WATUMISHI WA KARAKANA ZA TEMESA WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akizungumza na watumishi wa karakana za TEMESA wakati akifungua mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam.
HomeJamii

WATUMISHI WA KARAKANA ZA TEMESA WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akizungumza na watumishi wa karakana za TEMESA wakati akifun...

SERIKALI KUPANDA MITI MILIONI 280 KILA MWAKA ILI KUKABILIANA NA HALI YA JANGWA N
MAKAMU WA RAIS AFUNGA TAMASHA LA UELIMISHAJI NA UPIMAJI KWA WATOTO NA VIJANA KATIKA SIKU MAADHIMISHO YA MTOTO DAR
CRDB YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA ZAWADI







Baadhi ya watumishi wa karakana za TEMESA wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(hayupo Pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi hao Jijini Dar es Salaam.






Na Theresia Mwami TEMESA




Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme - TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu leo amefungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa karakana juu ya mfumo wa
utozaji gharama za matengenezo ya magari katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za uzalishaji na matengenezo za kila mwezi.

Dkt. Mgwatu amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuleta uwiano sawa katika gharama za matengenezo ya magari kwa karakana zote za TEMESA bila kujali
mikoa zilipo karakana hizo.


Aliongeza kuwa utaratibu utakaoelekezwa katika mafunzo hayo utasaidia kupunguza gharama za matengenezo ya magari ya serikali, suala linalolalamikiwa
na wateja wa TEMESA kwa muda mrefu sasa.

“Nataka sasa tuanze kutoza gharama za matengenezo ya magari kulingana na muda unaotumika kutengeneza gari husika (man hour), badala ya kutumia kigezo cha asilimia ya fedha iliyotumika kununulia vipuri kwa ajili ya
matengenezo ya magari, kwani baadhi ya vipuri ni ghali sana lakini hutumia muda mchache sana kuvifunga,” alisema Dkt. Mgwatu.





Dkt. Mgwatu alisema kuwa, kumekuwa na changamoto ya uwasilishaji wa taarifa za utendaji  kutoka katika
mikoa/vituo vya TEMESA, mara nyingi taarifa hizi hazifiki kwa wakati. Huku akisisitiza kuwa ni matumaini yake baada ya mafunzo hayo taarifa hizo zitakuwa
zikifika kwa wakati tena zikiwa sahihi.

Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Matengenezo, Mhandisi Sylivester Simfukwe alisema idara yake imejipanga kutoa huduma bora zinazokidhi
viwango hasa katika matengenezo ya magari ya serikali, ili kuhakikisha kuwa uzalishaji unaongezeka na kero za wateja zinakwisha.

 Aliongeza kuwa mafunzo kama hayo yatatolewa kwa wawakilishi wa karakana zote za TEMESA nchi nzima.

Mafunzo hayo elekezi juu ya Mfumo wa utozaji gharama katika karakana za TEMESA pamoja na mfumo wa utoaji taarifa za kila mwezi, yanafanyika
kwa siku 5 katika ukumbi wa MT. Depot, Dar es salaam na yamehusisha watendaji wa TEMESA kutoka mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na
Mtwara, pamoja na vituo vya MT. Depot na Kikosi cha Umeme.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WATUMISHI WA KARAKANA ZA TEMESA WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI.
WATUMISHI WA KARAKANA ZA TEMESA WAPATIWA MAFUNZO ELEKEZI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL_AT0ZuLwh1aavfpu2p27yDS6KCMNfZERm4h14u52UDS6YIIpGJjco6pJhUu54QVm6LAr-GRr9qVdguFf01rDKfIfmw4DHt_4gQG0Er8PCzjWqHHSvnXRkJXkippof8qwSswobnCwmvo/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiL_AT0ZuLwh1aavfpu2p27yDS6KCMNfZERm4h14u52UDS6YIIpGJjco6pJhUu54QVm6LAr-GRr9qVdguFf01rDKfIfmw4DHt_4gQG0Er8PCzjWqHHSvnXRkJXkippof8qwSswobnCwmvo/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/watumishi-wa-karakana-za-temesa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/watumishi-wa-karakana-za-temesa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy