WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dk...
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amewasili nchini Mauritius leo (Jumapili, Machi 19, 2017) kwa
ajili ya kumuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano wa
kuzindua Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur
Ramgoolam Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius
Mheshimiwa Vishnu Lutchmeenaraidoo.
Uzinduzi wa
jukwaa hilo unatarajiwa kufanyika kesho mjini Port Louis ambapo utawakutanisha
viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wanazuoni, wafanyabiashara pamoja na watu
kutoka kwenye asasi mbalimbali za kiraia barani Afrika.
Pamoja na
kuhudhuria mkutano huo, pia Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary
Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara kati ya
Tanzania na Mauritius litakalofanyika Machi 23, 2017.
Aidha, Waziri
Mkuu mara baada ya kumaliza mkutano huo anatarajia kutembelea maeneo maalumu ya
uwekezaji, viwanda vya sukari na nguo.
Waziri Mkuu
ameambatana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt.
Khalid
Salum Mohammed
na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa . Charles Mwijage pamoja na
maofisa wengine wa Serikali.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
JUMAPILI,
MACHI 19, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiogozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw.
Vishnu Lutchmeenaraidoo wakati alipopokelewa kwenye uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha
Rais John Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa
mjini Port Luis kuanzi Machi 20, 2017. (PICHA
NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw.
Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John
Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port
Luis kuanzi Machi 20, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritius, Bw.
Vishnu Lutchmeenaraidoo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Sir Seewoosagur Ramgoolam nchini Mauritius kumwakilisha Rais John
Pombe Magufuli katika Uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Africa mjini Port
Luis kuanzi Machi 20, 2017. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa.
COMMENTS