Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na anachukua nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na anachukua nafasi ya Bi. Halima Dendego.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kumbadilisha na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi. Christine Solomon Mndeme baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kumbadilisha na
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, kubadilishana na Dkt. Bilinith Mahenge anayehamia Dodoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe.Bi.Suzana Mlawi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe.Bi.Suzana Mlawi kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dorothy Mwanyika kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Vingozi wakati wa hafla ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Joseph Kizito Malongo kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhandisi Joseph Kizito Malongo kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Prof. Simon S. Msanjila kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Prof. Simon S. Msanjila kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Madini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya KilimoIkulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya KilimoIkulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe Dorothy Mwaluko kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe Dorothy Mwaluko kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Butamo Kasuka Phillipo kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Mhe. Butamo Kasuka Phillipo kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sahihi katika hati yake ya kiapo baadavya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Buchwaishaija
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe Nicholaus B. William kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli baada ya kumuapisha Mhe Nicholaus B. William kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Susana Mkap a kuwa Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Wizara ya Fedha na Mipango.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo baada ya kumuapisha Bi. Susana Mkap a kuwa Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Wizara ya Fedha na Mipango.
Waapishwa wakila kiapo cha miiko ya maadili ya vingozi wa umma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea machache
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma akiongea
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akitoa nasaha zake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Sehemu ya viongozi waandamizi wa nyanja mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu kiongozi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa mbalimbali pamoja na wale aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwapongeza viongozi aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28,
201
j47 na j488: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan wakiwapongeza viongozi aliowaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28,
2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikoo na naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu anayeshughulikia walemavu Mhe Stella Alex Ikupa akiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Mhe Nicholaus B. William aliyemuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28, 2017. Kulia ni mke wa Mhe. William Bi. Foster Mbuna.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 28,
201
Wazira wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akiteta jambo na Katibu Mkuu mpya wa wizara hiyo Prof. Adolf F. Mkenda (kati) na aliyekuwa Katibu Mkuu wizarani humo Dkt. Aziz Mlima. (PICHA ZOTE NA IKULU)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Oktoba 2017 amewaapisha Wakuu wa Mikoa 6, Makatibu Wakuu 4 na Naibu Makatibu Wakuu 7 aliowateua jana tarehe 26 Oktoba, 2017.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na viongozi wengine mbalimbali.
Wakuu wa mikoa walioapishwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Adam Kighoma Malima, Mkuu wa Mkoa Manyara Bw. Alexander Pastory Mnyeti, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Joackim Leonard Wangabo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel Lughumbi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Gasper Byakanwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Solomon Mndeme.
Awali Bi. Christina Solomoni Mndeme aliapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na baada ya kiapo Mhe. Rais Magufuli amefanya mabadiliko kwa kumhamisha kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge amehamishwa na sasa atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Makatibu Wakuu walioapishwa ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Kizito Malongo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Paul Mlawi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Dorothy Stanley Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Samwel Msanjila.
Naibu Makatibu Wakuu walioapishwa ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Dorothy Aidan Mwaluko, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi. Butamo Kasuka Phillip, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Didimu Kashililah na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susana Bernard Mkapa.
Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Joseph Rwegasira Bushweishaija, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Niclolaus William na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Viwanda) Bw. Ludovick James Nduhiye.
Akizungumza baada ya kuwaapisha, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi hao kuwatumikia wananchi vizuri kwa kutatua kero zinazowakabili na kuleta mabadiliko yatakayosaidia kuboresha maisha yao.
Ametolea mfano wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kuwa hatarajii kusikia wanafunzi vyuo vya elimu ya juu wamecheleweshewa mikopo kwa kuwa tayari Hazina imeshapeleka Shilingi Bilioni 147 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi ambao vyuo vinafunguliwa hivi karibuni.
“Nataka kila Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ajiulize amefanya nini kubadili maisha ya wananchi wa Mkoa wake ama Wilaya yake, nataka Makatibu Makuu na Naibu Makatibu Wakuu wakatatue kero zilizopo katika wizara zao” Amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda kufanya mabadiliko ya kiutendaji katika Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri diplomasia ya uchumi, kuhakikisha kila Balozi anayeiwakilisha Tanzania nje ya nchi anafanya kazi yenye kuleta manufaa kwa Tanzania na kuondoa watumishi wa waliopo katika Balozi mbalimbali duniani pasipo sababu za msingi za kuwepo kwao nje ya nchi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2017
COMMENTS