WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.
HomeJamii

WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.

Na Estom Sanga- Wadau wa Maendeleo wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia kwa ufanisi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelez...

JENGO LA ABIRIA KIWANJA CHA DODOMA KUBORESHWA
IGP SIMON SIRRO AFANYA UKAGUZI WA MRADI WA UJENZI MAKAO YA POLISI DODOMA
RC MAKONDA APOKEA TANI 120 ZA SARUJI KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA 27 VYA MKOA WA DAR





Na Estom Sanga-

Wadau wa Maendeleo wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia kwa ufanisi Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- Mpango ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya umaskini kwa Walengwa wake.

Wadau hao wa Maendeleo ambao wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na Walengwa na kushuhudia namna Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unavyotekelezwa, wamejionea namna Walengwa wanavyoendelea kuboresha maisha yao kwa kutumia fursa ya kujumuishwa kwenye shughuli za Mpango zilizoanza takribani miaka mitano iliyopita.

Katika maeneo walikotembelea ikiwemo, Zanzibar, Korogwe, Shinyanga, Kagera, na Manyara,wadau hao wa Maendeleo walioambatana na Maafisa wa serikali na wale wa TASAF wameshuhudia mafanikio makubwa katika sekta za elimu, afya, ujenzi wa nyumba, kilimo, ufugaji na miradi ya uchimbaji wa malambo ya maji na jitihada mpya za kuunda vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana miongoni mwa Walengwa ili kukuza zaidi uwezo wao kiuchumi.

Wadau hao wa Maendeleo pia wamevutiwa zaidi na namna Walengwa wa TASAF walivyoamua kwa hiari yao kutumia sehemu ya ruzuku wanayoipata kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii CHF-na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote wa mwaka katika kaya husika, huku katika maeneo mengi mahudhurio ya watoto wanaotoka kwenye Kaya za Walengwa yamekuwa mazuri ikilinganishwa na kabla ya kuanza kwa shughuli za Mpango.

Kutokana na mabadiliko chanya kwa Walengwa, Kumekuwa na mahitaji makubwa ya Wataalamu hususani wa Ugani ambao wanahitajika kusaidia jitihada za Walengwa hao wa TASAF kutekeleza miradi ya kiuchumi wanayoianzisha ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi, ng’ombe,nguruwe,bata, na kilimo kulingana na maeneo yao.

Aidha imebainika kuwa idadi kubwa ya Wananchi ambao hawakupata fursa ya kuorodheshwa kwenye shughuli za Mpango ,wangelipenda kupata fursa hiyo ili waweze pia kunufaika na huduma zitolewazo kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.Hata hivyo kwa nyakati tofauti Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amezungumzia dhamira njema ya serikali ya kuhakikisha kuwa Wananchi wote wanaostahili kunufaika na shughuli za Mpango wanafanya hivyo nchini kote. Amesema serikali itafanya hivyo pindi fedha zitakapapatikana.

Hii leo Wadau hao wa maendeleo kutoka taasisi zinazochangia utekelezaji wa Mpango huo wa kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA zilizoko katika vijiji zaidi ya ELFU TISA sawa na asilimia 70 ya vijiji vyote nchini, wanaendelea na Mkutano wao kwenye Ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wadau wa Maendeleo wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF. 

Baadhi ya Wadau wa Maendeleo na Maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaoendela kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es Salaam. 


Mmoja wa Maafisa wa TASAF, Peter Lwanda aliyeshika kipaza sauti, akiwasilisha taarifa ya ziara ya wadau waliotembelea mkoa wa Shinyanga kuona utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wakifuatilia taarifa inayowasilishwa na mmoja wa Maafisa waliotembelea maeneo ya utekelezwaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (hayupo pichani). 


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akijadiliana jambo na Kiongozi wa Shughuli za TASAF Benki ya Dunia Mohammed Muderis kwenye Mkutano wa Wadau.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.
WADAU WA MAENDELEO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpDgSwc2FbYzaOoZpBoyI5LnJ35lxKfg9MfTHzQ98b6Oxy6beiNCtNvok1XhElB7w8dVWE5gje3rnZZ46Xruwsnfa7W8M8QoMItwvE9wdpFwrCFHJBPpXFW3kKCXjUjQagImgF-0TNvjD5/s640/New+Picture+%25281%2529.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpDgSwc2FbYzaOoZpBoyI5LnJ35lxKfg9MfTHzQ98b6Oxy6beiNCtNvok1XhElB7w8dVWE5gje3rnZZ46Xruwsnfa7W8M8QoMItwvE9wdpFwrCFHJBPpXFW3kKCXjUjQagImgF-0TNvjD5/s72-c/New+Picture+%25281%2529.png
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wadau-wa-maendeleo-waipongeza-serikali.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/04/wadau-wa-maendeleo-waipongeza-serikali.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy