JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU Simu: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.t...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Aprili, 2018 amefungua jengo la mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF, ofisi ya makao makuu ya benki ya NMB Mjini Dodoma na matawi mawili ya benki hiyo.
Jengo la PSPF lenye ghorofa 11 lina ukubwa wa mita za mraba 15,741.60, limejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.56 na ndani ya jengo hilo ndimo benki ya NMB imefungua ofisi zake za makao makuu, tawi la benki kwa wateja maalum, na tawi la benki kwa wateja binafsi lililopewa jina la Kambarage kwa lengo la kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu amesema jengo hilo ambalo tayari limeshapata wapangaji kwa asilimia 98 wengi wao wakiwa ofisi za umma, linatarajiwa kuzalisha Shilingi Bilioni 4.7 kila mwaka na litarejesha fedha za uwekezaji ndani ya miaka 8 na kwamba katika juhudi hizo hizo za kuunga mkono Serikali kuhamia Dodoma PSPF inatekeleza mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba 500 za watumishi kwa ushirikiano na mfuko wa hifadhi ya jamii wa Watumishi Housing.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker amesema benki hiyo yenye matawi 218 ndio benki kubwa inayoendeshwa kwa faida hapa nchini na ikiwa na kiwango kidogo cha mikopo chechefu, imekuwa ikichangia katika bajeti ya nchi kupitia kodi na gawio ambapo mwaka jana imetoa gawio la Shilingi Bilioni 16.525 kila mwaka na katika sherehe hizo amechangia Shilingi Milioni 50 kwa maendeleo ya Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya Mke wa Baba wa Taifa Mhe. Mama Maria Nyerere, Mtoto wa Baba wa Taifa Bw. Makongoro Nyerere ameishukuru benki ya NMB kwa kutambua mchango wa Baba wa Taifa na kuamua tawi hilo liitwe jina lake la “Kambarage” na pia ametoa wito kwa vijana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais Magufuli.
“Mhe. Rais wewe chapa kazi, hawa wanaokushambulia na kukupinga hata wakati wa Baba wa Taifa walikuwepo na wengine walikimbilia nchi nyingine, wewe chapa kazi” amesisitiza Bw. Makongoro Nyerere.
Akihutubia kabla ya kufungua rasmi miradi hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza PSPF kwa kuwekeza katika jengo ambalo tayari limeshapata wapangaji na pia ameipongeza mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuitikia wito wa kuwekeza katika viwanda 16 ambavyo vitazalisha ajira na kuchangia katika uchumi wa nchi.
Mhe. Rais Magufuli amewatoa shaka wanachama na wafanyakazi wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa hatua ya Serikali kuunganisha mifuko hiyo na kubakiwa na mifuko miwili haitawaathiri bali ina lengo la kuongeza ufanisi.
Mhe. Rais Magufuli pia ameipongeza benki ya NMB kwa kazi nzuri inayofanya na kwa kuwafikishia huduma Watanzania wengi, lakini ametaka katika mwaka huu wa 2017/18 benki hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 32 iongeze gawio.
“Mwaka 2012/13 Benki ya NMB ilitoa gawio kwa Serikali la Shilingi Bilioni 10.805, mwaka 2013/14 ikatoa Shilingi Bilioni 14.301, mwaka 2014/15 ikatoa Shilingi Biliongi 16.525, mwaka 2015/16 ikatoa gawio hilohilo la Shilingi Bilioni 16.525 na mwaka 2016/17 ikatoa tena gawio hilohilo la Shilingi Bilioni 16.525, yaani miaka mitatu mfurulizo mnatoa gawio lilelile wakati mnatuambia faida ya benki imekua, nataka mnaoiwakilisha Serikali kwenye NMB mkaliangalie hili na gawio la mwaka 2017/18 liongezeke” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amejibu ombi lililotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde la kupunguzwa kwa tozo ya kodi katika mchuzi wa zabibu, na amewataka wadau wanaohusika wakiwemo wabunge kufanyia kazi ombi hilo kwa zao la zabibu na mazao mengine ya kilimo na mifugo hapa nchini ili tozo za kodi zisisababishe bidhaa za wazalishaji wa Tanzania kushindwa kushindana na bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi.
Mhe. Rais Magufuli pia amemshukuru Mtoto wa Baba wa Taifa Bw. Makongoro Nyerere kwa ujumbe wake kwa Watanzania hasa vijana na amemhakikishia kuwa Serikali anayoiongoza ipo imara na itaendelea kuwa imara kusimamia misingi ya kulijenga Taifa.
Ufunguzi wa miradi hiyo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Mawaziri, Makatibu Wakuu na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Dodoma
23 Aprili, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na
uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la
kitegauchumi mkoani Dodoma.
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na
uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la
kitegauchumi mkoani Dodoma.
Kilichomfanya
Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa
12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi
uliofanyika Aprili 23, 2018.
Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa
12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi
uliofanyika Aprili 23, 2018.
“Ninyi
mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na
mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga
mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja
na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF
mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na
kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” Alisema
Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda
sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni
miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea
chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Rais
pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.
pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.
“Nimefurahi
kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania,
ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira
wakati wa ujenzi.” Alipongeza.
kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania,
ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira
wakati wa ujenzi.” Alipongeza.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema,
PSPF ndio Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii kuweka kitegauchumi cha jingo mkoani
Dodoma na hivyo kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuhamia
makao makuu ya Nchi, mjini Dodoma.

Aidha
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
akielezea
historia ya uwekezaji huo alisema, Mfuko
ulipewa viwanja vya mradi huu na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu
(CDA) mwaka 2012 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuendeshea shughuli za Mfuko
pindi inapotokea dharura (business continuity) pamoja na kibiashara. Kazi ya usanifu
na ujenzi wa jengo hili lilianza Julai 2015 na kukamilika Januari 2018 na kwa
sasa jengo liko kwenye kipindi cha uangalizi (Defect Liability Period) ambacho
kitaisha Januari 2019. Gharama tarajiwa za mradi yaani “contract sum” ni
shilingi bilioni 37.02. Mpaka sasa Mfuko umeshalipa kiasi cha Shilingi za
Kitanzania bilioni 30.56.

Jengo hili lina minara miwili, mmoja ukiwa na ghorofa 11
na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60
pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni
kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara.
na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60
pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni
kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara.
“Hadi sasa jengo limepata wapangaji ambao kwa uchache ni
kama ifuatavyo; NMB Bank, AZANIA Bank, TIB Corporate Bank, Benki ya Kilimo, GIZ,
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TASAF, TANAPA, TBS, Gaming Board, PPRA, Makao
Makuu ya TARURA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi
wa Umma, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao hawa pamoja na wengine
wanafanya jengo kuwa limepangishwa kwa asilimia 98. Na kufikia leo Mfuko
umeshakusanya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 1.06 bilioni kutokana na malipo
ya pango na tunatarajia kukusanya kiasi
cha Shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka na kufikia miaka minane mradi utakua
umerejesha fedha zote zilizowekezwa.”Alibainisha Bw. Mayingu.

Rais akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Mhandisi Musa Iyombe, akitoa hotuba yake.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, (wakwanza kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Siro, wakati wa uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa PSPF
Mameneja wa PSPF
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Binilith Mahenge, (kushoto), akipokewa na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akiwasili kwenye eneo la tukio.
Rais, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wadhamini na wafanyakazi wa PSPF.
Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi.Costantina Martin, (kushoto), akibadilishana mawazo na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abass, (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Kikundi cha Sanaa kikitumbuiza kwenye hafla hiyo.
COMMENTS