MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 49 LA AFYA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 49 la Afya na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Madaktari Tanzania ulioanza na kufanyika kwenye hoteli ya  Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

HomeJamii

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 49 LA AFYA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliagiza Baraza la Mitihani kufanya uhakiki haraka ili...

TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE
WIZARA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUFANYIA MKUTANO KWA NJIA YA VIDEO
CAG KUCHUNGUZA MAPATO YA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA-MAJALIWA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliagiza Baraza la Mitihani kufanya uhakiki haraka ili wataalamu wa Sekta za Afya wapangiwe vituo.
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 49 la Afya na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama Cha Madaktari, alisema “Tangu tuingie madarakani serikali imeweza kutoa vibali vya ajira mpya vipatavyo 3,410 kwa awamu mbili, awamu ya kwanza vibali vya madaktari 258 na awamu ya pili vibali 3,150 kwa wataalamu wa kada ya afya na taratibu za ajira kwa wataalamu hawa 3150 zimekamilika na imebakia hatua ya uhakiki wa vyeti katika Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)” Hivyo Makamu wa Rais alielekeza Baraza la Mitihani la Taifa kukamilisha uhakiki huo haraka ili wataalamu hao waweze kupangiwa maeneo ya kazi na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Makamu wa Rais aliwapongeza Chama cha Madaktari kwa kuweza kuandaa Kongamano la 49 na kuweka historia ya kuandaa Makongamano tangu mwaka 1965.
Kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “ Malengo ya Maendeleo Endelevu: Uweledi wa Kitaaluma na Utoaji Bora wa Huduma za Afya Nchini Tanzania.” Mada hii ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza kwa vitendo wajibu wake wa kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa huduma za afya zenye viwango na zinazokidhi mahitaji alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alisema Serikali imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuandaa muswada wa Bima ya Afya kwa wote kwani itasaidia sana kukabiliana na ongezeko la gharama za matibabu.
Aliendelea kusema kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha kadri ya uwezo unavyopatikana kwa watumishi wa kada ya afya.
Vile vile Makamu wa Rais alisema Serikali tayari imeshashughulikia suala lakuwa na mtihani mmoja kwa watahiniwa wote wa vyuo vyote vya afya nchini ambapo suala hili limezingatiwa katika sheria ya madaktari, madaktari wa weno na wataalamu wa afya shirikishi iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Septemba, 2017.
Makamu wa Rais alisema Serikali imeanza utaratibu wa kununua moja kwa moja Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupunguza gharama zilizokuwa zinatumika.
Mwisho Makamu wa Rais aliwapongeza na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na mapendekezo yao atayachukua na kumfikishia Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Kwa Upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alihimiza weledi lakini pia alikemea vitendo vya Viongozi wengine kuwachukulia hatua madaktari na badala yake wafuate utaratibu uliowekwa.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo. 






Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 49 LA AFYA
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA 49 LA AFYA
https://i.ytimg.com/vi/vI1X4vnVH08/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/vI1X4vnVH08/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/makamu-wa-rais-afungua-kongamano-la-49_25.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/makamu-wa-rais-afungua-kongamano-la-49_25.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy