TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE
HomeJamii

TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE

Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha hudum...

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA TANESCO SACCOS LTD WAFANYIKA JIJINI DAR
NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AFANYA ZIARA UJENZI WA BARABARA YA JUU TAZARA
KUMBUKUMBU YA MIAKA 18 YA KIFO CHA HAYATI MWALIMU KAMBARAGE NYERERE..
Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa  kwa huduma hizo zitapokuwa tayari.
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
"Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano", imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo - Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah Mrisho -  wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.              
"Gloval TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili - kama zingekuwepo - na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya," alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard  Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa. 
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
"Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii", alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV,  ambazo zinaongoza kwa mbali kwa kutazamwa na watu wengi nchini na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA, kati ya vituo mtandao  takriban 51 vilivyopata barua hiyo.

Ankal Issa Michuzi wa Michuzi TV, Millard Ayo (wa pili kulia), Askofu wa Ayo TV na Abdallah Mrisho wa Global TV (wa pili kushoto) wakitoka makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano walikoitwa kuchukua barua zao zinazowazuia kuendelea kutoa huduma za TV mtandao hadi hapo kanuni za usajili na leseni utapokamilika.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE
TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgL_fkRmbYGv-OGCX_X69SGIIvt56YPs5Do1p4TjQ4dXOlJK42jDblosZIWKhqD5K-t7wpWYmi-mDts5DGDi8M50HNSRW2WYPwnmgG3evSG60yFuD7aJCJ9oCxblA0wb2i-2ECvdeiQvxw/s640/unnamed+%25283%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgL_fkRmbYGv-OGCX_X69SGIIvt56YPs5Do1p4TjQ4dXOlJK42jDblosZIWKhqD5K-t7wpWYmi-mDts5DGDi8M50HNSRW2WYPwnmgG3evSG60yFuD7aJCJ9oCxblA0wb2i-2ECvdeiQvxw/s72-c/unnamed+%25283%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/tcra-yazipiga-pini-michuzi-tv-ayo-tv-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/tcra-yazipiga-pini-michuzi-tv-ayo-tv-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy