MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI
HomeJamii

MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI

Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH),  Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na wahudumu  wa  Afya katika ...

MHE. RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA ENEO LA MSAMVU MOROGORO
SKAUTI TANZANIA YATIMIZA MIAKA 100, MAKAMU WA RAIS ATOA NISHANI KWA VIONGOZI WA JUU WASTAAFU
NAIBU WAZIRI WAMBURA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA HABARI NA MTANDAO


Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH),  Profesa  Lawrence Museru leo amekutana na wahudumu  wa  Afya katika hospitali hiyo pamoja na mambo mengine  amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili. Pia mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi  ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika  mkutano  na baadhi ya wahudumu wa afya  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Profesa Museru  amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali, lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.

" Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora  na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana  ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.

Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda  14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo  ili kuongeza  ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao.
Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo.  Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Mtemi Sufiani Baruani, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala, Leila Komba,  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Hedwiga Swai wakiwasikiliza wahudumu wa hospitali hiyo katika mkutano uliowahusisha viongozi hao. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa jengo la maabara kuu.
 
 Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. 
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa hospitali hiyo akizungumza na wahudumu leo katika mkutano.
 
  Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo, Joseph Oloch akizungumza kwenye mkutano huo leo.
 Baadhi ya wahudumu hao wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru leo.
 Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo leo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI
MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhffsBaJZjp5bSZ4jh_rjqvEU69asUbrAyOUI3sZDvOIANdQAwJRPLRjLJAl-B4RtSXZm7JNtr_3VLVunDXpQZhYuT9KW38hoOG9UEPVdrQ3PmzMdlRw9Ec8Oe4lrrQU8k3xKPGeL2VaIVJ/s640/0009.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhffsBaJZjp5bSZ4jh_rjqvEU69asUbrAyOUI3sZDvOIANdQAwJRPLRjLJAl-B4RtSXZm7JNtr_3VLVunDXpQZhYuT9KW38hoOG9UEPVdrQ3PmzMdlRw9Ec8Oe4lrrQU8k3xKPGeL2VaIVJ/s72-c/0009.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/mkurugenzi-muhimbili-tutaendelea.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/mkurugenzi-muhimbili-tutaendelea.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy