WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapa...
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL).
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamis, Februari 9, 2017)
alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.
“Nitamuagiza CAG
aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia
mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika
hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio
kwa manufaa ya Taifa. Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake
waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.
“Vitu vingi vinavyoenda manual ni rahisi kufa. Serikali
tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu
tumepata mafanikio,”amesema. Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha
zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti
upotevu wa mapato.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo
kuhakikisha wanazingaria ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze
wateja.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
S. L. P.
980,
DODOMA.
ALHAMIS,
FEBRUARI 9, 2017
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia
mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9,
2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa
Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi
Ladislaus Matindi.

Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL. Mhandisi
Ladislaus Matindi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia)
kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati
alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini
Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi
wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu
wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
COMMENTS