HomeJamii

MAKAMU WA RAIS KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA WILAYA YA MUHEZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwezesha kupatikana kwa shilingi bilioni moja n...

MHANDISI METHEW MTIGUMWE AWASHUKURU WADAU WOTE WALIOSHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA –NANE NANE MWAKA 2017
WAZIRI MKUU AWAONYA WATU WANAOCHUKUA DAWA KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI NA KUZIPELEKA KATIKA MADUKA YAO
GRACA MACHEL ATEMBELEA WAJASIRAIMALI WALIOJUMUIKA KATIKA MKUTANO WA WOMEN ADVANCING AFRICA










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwezesha kupatikana kwa shilingi bilioni moja na milioni mia saba kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais aliwapongeza uongozi wa Wilaya ya Muheza na mkoa wa Tanga pamoja na wananchi kwa kuamua kujenga hospitali yao ya wilaya ili kuboresha hali ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu wa Rais alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuimarisha ubora wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutoka kiwango cha vifo 66 kati ya vizazi hai 1,000 hadi kufikia kiwango cha angalau vifo 40 kati ya vizazi hai 1,000. Aidha, Serikali imedhamiria kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kutoka 556 kwa mwaka 2017 katika vizazi hai 100,000 hadi kufikia 292 ifikapo mwaka 2020.
Sambamba na hilo Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo tuna mkakati wa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya Vituo vya afya 208 ili kuimarisha utolewaji wa huduma mbalimbali za afya.
Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa mkoa pamoja na wa Wilaya ya Muheza kuupa kipaumbele mradi huu wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuhakikisha wanaweka mradi huu katika bajeti zinazokuja pamoja na kutafuta wahisani wengine wa ndani na nje ya nchi ili kuwezesha ujenzi wa hospitali hiyo kukamilika kwa haraka.
Makamu wa Rais aliwashukuru Wadau wote walioshiriki na kuomba kila mmoja wetu achangie kwa uwezo na nafasi yake ili hospitali ya Wilaya ya Muheza ikamilike mapema.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe. Adadi Rajabu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuwezesha kufanikisha kupatikana kwa mchango mkubwa ambao hawakuutegemea na kuahidi ili kuuenzi mchango huu na mapenzi ya  Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa wana Muheza basi watahakikisha hospitali hiyo au jengo lolote lile la Hospitali hiyo linapewa jina la Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA WILAYA YA MUHEZA
MAKAMU WA RAIS KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA WILAYA YA MUHEZA
https://i.ytimg.com/vi/ndHEkvwAw2o/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/ndHEkvwAw2o/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-kuchangia-ujenzi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-kuchangia-ujenzi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy