Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (kulia) akizungumza na wabunge na baad...
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta
Nditiye (kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi
na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa
wakiangalia sanamu mtu wa kabila la Kimasai iliyochongwa kwa kutumia mti
aina ya Mpingo kabla ya Wabunge wa kamati hiyo kuanza kutembelea
Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta
Nditiye (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Eng. Ramo Makani (wa tatu kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na wabunge na
baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa
wakiangalia zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale wakati
Wabunge wa kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii walipokuwa wakitembelea
Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta
Nditiye (kulia) akitia saini kwenye kitabu cha Wageni
akishuhudiwa na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na
Utalii pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii
wakiwa kwenye chumba maalumu (strong room) cha kuhifadhia urithi wa
utamaduni wa thamani kubwa kama zamadamu (hominine remains), masalia ya
akiolojia, historia pamoja na sanaa ya ethnographic) jana walipotembelea
Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani (kushoto) akitia
msisitizo jambo kwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi
na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (katikati) akiwa pamoja na Mbunge wa
kamati hiyo, Mhe, Shabani Shekilindi (kulia) mara baada ya
kumaliza ziaraya kutembelea kijiji cha Makumbusho cha Kijitonyama,
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akiwaelezea Wabunge wa
Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii kuhusu meli ya kivita ya iliyozama
baharini iliyotumiwa na jeshi la Kijerumani wakati wa vita vya kwanza
duniani (1914-1919).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi
akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na
Utalii, Eng. Atashasta Nditiye wakati wakielekea kuangalia Nyumba ya
wahehe iliyopo kijiji cha Makumbusho cha Kijitonyama, jijini Dar es
Salaam, ( Picha na Lusungu Helela- WMU)
COMMENTS