JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI Simu: 255-22-2114615, 211906-12 Bar...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara yapokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima leo amepokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video (Video Conference Facilities) kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP).
Baada ya kupokea msaada huo, Balozi Mlima aliishukuru UNDP kwa msaada huo ambao alieleza kuwa utasaidia shughuli za Wizara katika ofisi mpya ya Wizara mjini Dodoma. Alisema msaada huo ni wa pili kwa Wizara katika muda mfupi ambapo awali UNDP ilitoa ngamizi, printers na cameras.
“Tunamshukuru Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ambaye ndio alianzisha suala hili na kuongea nanyi na kulisimamia bila kuchoka hadi leo vifaa vinapatikana” “Kwa kweli ni mtu ambaye wakati wote anapenda mambo anayoyasimamia yanatokea” Katibu Mkuu alimwambia Mkurugenzi wa UNDP nchini Tanzania, Bi. Awa Dabo.
Kwa upande wake Bi. Dabo baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa mazungumzo kuhusu maombi ya msaada huo yalianza tokea mwaka 2014 lakini kwa uwezo wa mungu vifaa hivyo leo vimekabidhiwa rasmi Wizarani. Alielezea matumani yake kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa Wizara na pia utaboresha na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali na UNDP.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 09 Februari 2017.
COMMENTS