PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO
HomeJamii

PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa...

DKT MWANJELWA AAGIZA WATUMISHI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA
WANAFUNZI 11,481 WAPATA MIKOPO AWAMU YA PILI 2017-2018
MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA ANTIBIOTICS KIHOLELA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wa pili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, (wa pili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango wa PPF kwenye Jamii.




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


MFUKO wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.

Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.


Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu aliungana na Bodi ya
Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya Afya 16 nchini vitakavyonufaika na msaada wa vifaa hivyo.
 

Mhe. Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.


“Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.


Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, alisema, msaada wa vifaa hivyo ni moja ya majukumu ya Mfuko kusaidia jamii (CSR), hivyo PPF itatoa msaada kama huo kwa hospitali na vituo vya afya vingine 15.

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula,
 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Juma Mhina.






Waziri Mhe. Mhagama akitoa hotuba yake




Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Khijjah, akitoa hotuba yake




Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akitoa hotuba yake


Wakurugenzi wa PPF; Waliovaa suti kutoka kushoto, Mkurugenziwa Mifumo ya Kompyuta,  Riobert Mtendamema, Mkurugenzi wa Fedha, Martin Mmari, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Steven Alfred na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa




Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, akitoa hotuba yake


Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Sara Barahomoka.




Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Aggrey Mlimuka (katikati), Mjumbe wa Bodi, Amelye Nyembe na Mkurugebnzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Longido, Juma Mhina, wakiwa kwenye hafla hiyo


Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa PPF, Bi. Uphoo Swai, (katikati), akiwa na mwenyeji wa Longido wakifuatilia hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Martin Mmari




Wakurugenzi na Mameneja wa PPF pamoja na watumishi wa Halmashauriya Wilaya ya Longido wakijumuika kwenye hafla hiyo


Wananchi wa Longido walikuwa ni mashahidi wakati wa kupokea msaada huo


Mkurugenzi Mkuu wa PPF naujumbe wake wakipokewa na viongozi wa Kituo cha Afya Lungido walipowasili kukabidhi msaada huo.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO
PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgjz_ZuVXzM92AVcIeycyrZncCE0JNbewANLPJ-rxwUsJAM813X838UvqxYOgZuQfJFG24qn8cD4Abf-F61RmoH99MFxEgr5FmsuAFk32fEHUhT7F4ePSeN-JyUCom2rjUhfP2rDfARbA/s640/Longido2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgjz_ZuVXzM92AVcIeycyrZncCE0JNbewANLPJ-rxwUsJAM813X838UvqxYOgZuQfJFG24qn8cD4Abf-F61RmoH99MFxEgr5FmsuAFk32fEHUhT7F4ePSeN-JyUCom2rjUhfP2rDfARbA/s72-c/Longido2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/ppf-yakabidhi-vifaa-tiba-katika-kituo.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/ppf-yakabidhi-vifaa-tiba-katika-kituo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy