Na Bashir Yakub. Una mahusiano na mwanaume au mwanamke ambaye kimsingi mpo katika uchumba. Unampa zawadi nyingi naye anakupa za...
Una
mahusiano na mwanaume au mwanamke ambaye kimsingi mpo katika uchumba.
Unampa zawadi nyingi naye anakupa zawadi. Mnayo ahadi ya kufunga ndoa na
kuishi kama mme na mke . Na kwasababu hiyo unajitoa sana kimatumizi kwa
mtu huyo.
Lakini
katika mazingira usiyoyaelewa unaona sasa mambo hayaendi vizuri.
Hayaendi vizuri katika kiwango ambacho sasa mahusiano yamevunjika
kabisa. Hakuna tena mahusiano. Au bado yapo lakini kwa mambo
unayofanyiwa unaona kabisa hutakiwi tena.
Kumbuka
huko nyuma umegharamia sana. Umegharamia kwa fedha na mali. Swali ni je
vitu hivi haviwezi kurudishwa ?. Vitu hivi haviwezi kufidiwa ?. Na je
sheria imeongelea kuhusu jambo hili ?.
Majibu
ya maswali haya yote ni ndiyo. Ni ndiyo, na gharama pamoja nazo zawadi
zinaweza kurejeshwa. Unaweza kushangaa kuona sheria imeongelea hata
mambo ya uchumba lakini ndio ukweli.
Wengi
tunaijua sheria katika kuongelea wizi, dhamana, mikataba, mirathi, ndoa,
na mengine. Lakini ni vyema tukajua kuwa sheria ni pana na imeongelea
mambo mengi mno. Hili la uchumba nalo ni sehemu ya yaliyoongelewa.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com.
COMMENTS