MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MANUNUZI YA HISA KWA NJIA YA MTANDAO
HomeJamii

MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MANUNUZI YA HISA KWA NJIA YA MTANDAO

Mkuu wa kitengo cha Masoko na  Ubunifu , Deogratius Lazari Mosha akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) Kampun...

MPAKA MAFUTA WA KANISA LA SILOAM TANZANIA, AMFANYIA MAOMBI YA BARAKA KUHANI WA KANISA HILO NCHINI KENYA KUFUATIA KUWA MBUNGE NCHINI HUMO
MAPADRI VIONGOZI WA JIMBO LA RUANGWA MKOA WA LINDI WASAFIRI KWENDA KUHIJI ISRAEL, JORDAN NA PALESTINA
WAKAZI WA DAR ES SALAAM WAJITOKEZA KUFANYA USAFI COCO BEACH MAADHIMISHO YA USAFI WA FUKWE DUNIANI

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu, Deogratius Lazari Mosha akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani)
Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE)  kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa  Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu  Bwana. Deogratius Lazari Mosha,  Leo 13/03/2017 amewaambia waandishi wa habari kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la  Dar es Salaam(DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa  za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali  la mitaji (primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.
Akifafanua hili Bw. Deogratius Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Bw. Deogratius Lazari ameongeza kwamba baada ya hatua ya uanishaji wa hisa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye  nambari ya kumbukumbu ya malipo, idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili kukamilisha  malipo haya mteja  atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo aliye karibu naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe aliopokea kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa risiti pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu zake.
Kwa kuongezea Bw. Deogratius Lazari ameeleza kwamba mfumo huu rafiki unamwezesha mteja kushiriki manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake (Mfano, Mteja Anaweza kila siku akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au zaidi). Pamoja na mwakala wa Maxmalipo mteja anaweza  kulipia kwa kutumia mitandao ya simu.
Mfumo huu wa kununua hisa kwa simu za kiganjani  ( *150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es Salaam(DSE)  na ni mfumo rasmi wa kuuza na kununua hisa kwenye soko la hisa .
Bw. Deogratius Lazari ametoa wito kwa watanzania kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema  kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo  walioko nchi nzima  takribani Mawakala Elfu kumi na sita .
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MANUNUZI YA HISA KWA NJIA YA MTANDAO
MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MANUNUZI YA HISA KWA NJIA YA MTANDAO
https://lh4.googleusercontent.com/O2l9VAG40zYvXzB1YR9EMLIHq8hj9atgE_rbFjcQqLs1_VtckK19c8E74-5nQkLrXASYthtos6cBPqctjn3scA3gGHxikeGhZBBD8xp9aFV2bITcSEdPzNnBAZwV0qWcKhK1seFdIldwBymz3A
https://lh4.googleusercontent.com/O2l9VAG40zYvXzB1YR9EMLIHq8hj9atgE_rbFjcQqLs1_VtckK19c8E74-5nQkLrXASYthtos6cBPqctjn3scA3gGHxikeGhZBBD8xp9aFV2bITcSEdPzNnBAZwV0qWcKhK1seFdIldwBymz3A=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/maxcom-africa-maxmalipo-inawakaribisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/maxcom-africa-maxmalipo-inawakaribisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy