MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
HomeJamii

MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza ...


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
  (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya
Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa
 Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi
hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea
katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.


 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru
Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa
  magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya
Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa
  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
 
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston
Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi
hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Suleiman Msuya

NAIBU Waziriwa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni amesema Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wakuu wa magereza nchini ambao watashindwa kutimiza dhana ya uzalishaji mali ambayo ni agizo la Rais John Magufuli.

Aidha, Jeshi la Magereza Tanzania limetaja changamoto tano kuu ambazo zinakabili jeshi hilo hali ambayo inakwamisha ufanisi katika mipango yao.

Masuani alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa wakuu wa vituo vya magereza
Tanzania Bara unaofanyika katika Bwalo la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri alisema iwapo wakuu wa magereza watatumia wafungwa waliopo uzalishaji utaongezeka hivyo kuondokana na tabia ya kulalamika ufinyu wa bajeti.

Alisema pamoja na vigezo mbalimbali vya kupima wakuu wa magereza kigezo kingine kitakuwa ni kuangalia kasi ya uzalishaji kwa eneo husika.

Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia
fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.

“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,”
alisema.

Naibu waziri alisema anaamini kupitia jeshi hilo ajiraz itaongezeka, uchumi utakuwa na maendeleo ya nchi yatapatikana kwa haraka hivyo lengo la 2025 kukamilika.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali Magereza, Dk. Juma Malewa alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ufinyu wabajeti, madeni ya watumishi, makaziduni, ukosefu wa posho na vitendea kazi kama usafiri.

Alisema katika kutatua changamoto ya usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.

Dk. Malelwa alisema pia wameanza kutatua changamoto ya makazi ambapo Rais Magufuli ametoa sh. bilioni
10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 320 katika kambi ya Ukonga.

Kamishna Jenerali Malelwa
alisema hadi sasa wamepokea sh. Bilioni 5 ambazo zimeanza kutumika kujenga nyumba
hizo 320 zinazojengwa naWakala wa Majengo nchini (TBA).

Alisema wao wamejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inapatikana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivyo utatuzi wa changamoto hizo utakuwa suluhu sahihi kwao.

“Tumedhamiria kuongeza uzalishaji na kufufua viwanda mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini tunaomba changamoto nilizo zitaja zitatuliwe kwa wakati,” alisema.

Akizungumzia dhana hiyo ya viwanda Mkurugenzi waViwanda, Naibu Kamishna wa Magereza Edith Mallya alisema utekelezaji wa agizo la Serikali umeanza katika baadhi ya viwanda kama MbigiriMorogoro
na Karanga.









































Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwUfkW5xTey97WTTOjX15s1-G1vPlHG-zZzvD2batcXGeFF8FOE2Ou4_ztjngdE1NzlgdoPzaHVrmmt8Qz8IYytcLvEazIgcYGi8qv9XRKdIMB4AH9q7pNzvhsJNo4xKAqhrrNhWgTkuS8/s640/PIX+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgwUfkW5xTey97WTTOjX15s1-G1vPlHG-zZzvD2batcXGeFF8FOE2Ou4_ztjngdE1NzlgdoPzaHVrmmt8Qz8IYytcLvEazIgcYGi8qv9XRKdIMB4AH9q7pNzvhsJNo4xKAqhrrNhWgTkuS8/s72-c/PIX+1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/masauni-awataka-maafisa-magereza.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/masauni-awataka-maafisa-magereza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy